Maombolezo 3:58-66
Maombolezo 3:58-66 Biblia Habari Njema (BHN)
“Umenitetea katika kisa changu ee Mwenyezi-Mungu, umeyakomboa maisha yangu. Umeuona uovu niliotendewa ee Mwenyezi-Mungu, uniamulie kwa wema kisa changu. Umeuona uovu wa maadui zangu, na mipango yao yote ya hila dhidi yangu. “Umesikia matukano yao ee Mwenyezi-Mungu, na mipango yao yote ya hila dhidi yangu. Maneno na mawazo ya maadui zangu siku nzima ni juu ya kuniangamiza mimi. Wakati wote, wamekaa au wanakwenda, mimi ndiye wanayemzomea. Uwalipize, ee Mwenyezi-Mungu kadiri ya hayo matendo yao, kadiri ya mambo waliyotenda wenyewe. Uipumbaze mioyo yao, na laana yako iwashukie. Uwafuatie kwa hasira, uwaangamize, uwafanye watoweke ulimwenguni.”
Maombolezo 3:58-66 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ee BWANA umenitetea mateto ya nafsi yangu; Umeukomboa uhai wangu. Umekuona kudhulumiwa kwangu, Ee BWANA; Unihukumie neno langu. Umekiona kisasi chao chote, Na mashauri yao yote juu yangu. Ee BWANA, umeyasikia matukano yao, Na mashauri yao yote juu yangu; Midomo yao walioinuka juu yangu Na maazimio yao juu yangu mchana kutwa. Uangalie kuketi kwao, na kuinuka kwao; Wimbo wao ndio mimi. Utawalipa malipo, Ee BWANA, Sawasawa na kazi ya mikono yao. Utawapa ushupavu wa moyo; Laana yako juu yao. Utawafuatia kwa hasira, na kuwaangamiza Wasiwe tena chini ya mbingu za BWANA.
Maombolezo 3:58-66 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ee BWANA umenitetea katika kisa cha nafsi yangu; Umeukomboa uhai wangu. Umekuona kudhulumiwa kwangu, Ee BWANA; Unihukumie neno langu. Umekiona kisasi chao chote, Na mashauri yao yote juu yangu. Ee BWANA, umeyasikia matukano yao, Na mashauri yao yote juu yangu; Midomo yao walioinuka juu yangu Na maazimio yao juu yangu mchana kutwa. Uangalie kuketi kwao, na kuinuka kwao; Wimbo wao ndio mimi. Utawalipa malipo, Ee BWANA, Sawasawa na kazi ya mikono yao. Utawapa ushupavu wa moyo; Laana yako juu yao. Utawafuatia kwa hasira, na kuwaangamiza Wasiwe tena chini ya mbingu za BWANA.
Maombolezo 3:58-66 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Ee Bwana, ulichukua shauri langu, ukaukomboa uhai wangu. Umeona, Ee BWANA, ubaya niliotendewa. Tetea shauri langu! Umeona kina cha kisasi chao, mashauri yao yote mabaya dhidi yangu. Ee BWANA, umesikia matukano yao, mashauri yao yote mabaya dhidi yangu: kile adui zangu wanachonongʼona na kunungʼunikia dhidi yangu mchana kutwa. Watazame! Wakiwa wameketi au wamesimama, wananidhihaki katika nyimbo zao. Uwalipe kile wanachostahili, Ee BWANA, kwa yale ambayo mikono yao imetenda. Weka pazia juu ya mioyo yao, laana yako na iwe juu yao! Wafuatilie katika hasira na uwaangamize kutoka chini ya mbingu za BWANA.