Maombolezo 3:45-66
Maombolezo 3:45-66 Biblia Habari Njema (BHN)
Umetufanya kuwa takataka na uchafu miongoni mwa watu wa mataifa. “Maadui zetu wote wanatuzomea. Kitisho na hofu vimetuandama, tumepatwa na maafa na maangamizi. Macho yangu yabubujika mito ya machozi kwa sababu ya kuangamizwa kwa watu wangu. “Machozi yatanitoka bila kikomo, mpaka Mwenyezi-Mungu kutoka huko mbinguni aangalie chini na kuona. Nalia na kujaa majonzi, kuona yaliyowapata kina mama wa mji wangu. “Nimewindwa kama ndege na hao wanichukiao bila sababu. Walinitupa shimoni nikiwa hai na juu yangu wakarundika mawe. Maji yalianza kunifunika kichwa, nami nikafikiri, ‘Huu ni mwisho wangu.’ “Kutoka chini shimoni nilikulilia ee Mwenyezi-Mungu. Wewe umenisikia nikikulilia: ‘Usiache kusikia kilio changu cha msaada bali unipatie nafuu.’ Nilipokuita ulinijia karibu ukaniambia, ‘Usiogope!’ “Umenitetea katika kisa changu ee Mwenyezi-Mungu, umeyakomboa maisha yangu. Umeuona uovu niliotendewa ee Mwenyezi-Mungu, uniamulie kwa wema kisa changu. Umeuona uovu wa maadui zangu, na mipango yao yote ya hila dhidi yangu. “Umesikia matukano yao ee Mwenyezi-Mungu, na mipango yao yote ya hila dhidi yangu. Maneno na mawazo ya maadui zangu siku nzima ni juu ya kuniangamiza mimi. Wakati wote, wamekaa au wanakwenda, mimi ndiye wanayemzomea. Uwalipize, ee Mwenyezi-Mungu kadiri ya hayo matendo yao, kadiri ya mambo waliyotenda wenyewe. Uipumbaze mioyo yao, na laana yako iwashukie. Uwafuatie kwa hasira, uwaangamize, uwafanye watoweke ulimwenguni.”
Maombolezo 3:45-66 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Umetufanya kuwa takataka, na vifusi Katikati ya mataifa. Juu yetu adui zetu wote Wametupanulia vinywa vyao. Hofu imetujilia na shimo, Ukiwa na uharibifu. Jicho langu lachuruzika mito ya maji Kwa ajili ya uvunjifu wa binti ya watu wangu. Jicho langu latoka machozi lisikome, Wala haliachi; Hata BWANA atakapoangalia Na kutazama toka mbinguni. Jicho langu lanitia huzuni nafsini mwangu, Kwa sababu ya binti zote za mji wangu. Walio adui zangu bila sababu Wameniwinda sana kama ndege; Wameukatilia mbali uhai wangu gerezani, Na kutupa jiwe juu yangu. Maji mengi yalipita juu ya kichwa changu, Nikasema, Nimekatiliwa mbali. Naliliitia jina lako, BWANA, kutoka lile shimo Liendalo chini kabisa. Ukaisikia sauti yangu; usifiche sikio lako Ili usisikie pumzi yangu, kwa kilio changu. Ulinikaribia siku ile nilipokulilia; Ukasema, Usiogope. Ee BWANA umenitetea mateto ya nafsi yangu; Umeukomboa uhai wangu. Umekuona kudhulumiwa kwangu, Ee BWANA; Unihukumie neno langu. Umekiona kisasi chao chote, Na mashauri yao yote juu yangu. Ee BWANA, umeyasikia matukano yao, Na mashauri yao yote juu yangu; Midomo yao walioinuka juu yangu Na maazimio yao juu yangu mchana kutwa. Uangalie kuketi kwao, na kuinuka kwao; Wimbo wao ndio mimi. Utawalipa malipo, Ee BWANA, Sawasawa na kazi ya mikono yao. Utawapa ushupavu wa moyo; Laana yako juu yao. Utawafuatia kwa hasira, na kuwaangamiza Wasiwe tena chini ya mbingu za BWANA.
Maombolezo 3:45-66 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Umetufanya kuwa takataka, na vifusi Katikati ya mataifa. Juu yetu adui zetu wote Wametupanulia vinywa vyao. Hofu imetujilia na shimo, Ukiwa na uharibifu. Jicho langu lachuruzika mito ya machozi Kwa sababu ya kuharibiwa kwa binti zangu. Jicho langu latoka machozi lisikome, Wala haliachi; Hata BWANA atakapoangalia Na kutazama toka mbinguni. Jicho langu lanitia huzuni nafsini mwangu, Kwa ajili ya kuangamizwa kwa binti wa watu wangu. Walio adui zangu bila sababu Wameniwinda sana kama ndege; Wameukatilia mbali uhai wangu gerezani, Na kutupa jiwe juu yangu. Maji mengi yalipita juu ya kichwa changu, Nikasema, Nimekatiliwa mbali. Nililiitia jina lako, BWANA, kutoka lile shimo Liendalo chini kabisa. Ukaisikia sauti yangu; usifiche sikio lako Ili usisikie pumzi yangu, kwa kilio changu. Ulinikaribia siku ile nilipokulilia; Ukasema, Usiogope. Ee BWANA umenitetea katika kisa cha nafsi yangu; Umeukomboa uhai wangu. Umekuona kudhulumiwa kwangu, Ee BWANA; Unihukumie neno langu. Umekiona kisasi chao chote, Na mashauri yao yote juu yangu. Ee BWANA, umeyasikia matukano yao, Na mashauri yao yote juu yangu; Midomo yao walioinuka juu yangu Na maazimio yao juu yangu mchana kutwa. Uangalie kuketi kwao, na kuinuka kwao; Wimbo wao ndio mimi. Utawalipa malipo, Ee BWANA, Sawasawa na kazi ya mikono yao. Utawapa ushupavu wa moyo; Laana yako juu yao. Utawafuatia kwa hasira, na kuwaangamiza Wasiwe tena chini ya mbingu za BWANA.
Maombolezo 3:45-66 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Umetufanya takataka na uchafu miongoni mwa mataifa. “Adui zetu wote wamefumbua vinywa vyao wazi dhidi yetu. Tumeteseka kwa hofu kuu na shida ya ghafula, uharibifu na maangamizi.” Vijito vya machozi vinatiririka kutoka machoni mwangu, kwa sababu watu wangu wameangamizwa. Macho yangu yatatiririka machozi bila kukoma, bila kupata nafuu, hadi BWANA atazame chini kutoka mbinguni na kuona. Lile ninaloliona huniletea huzuni nafsini kwa sababu ya wanawake wote wa mji wangu. Wale waliokuwa adui zangu bila sababu wameniwinda kama ndege. Walijaribu kukomesha maisha yangu ndani ya shimo na kunitupia mawe; maji yalifunika juu ya kichwa changu, nami nikafikiri nilikuwa karibu kukatiliwa mbali. Nililiitia jina lako, Ee BWANA, kutoka vina vya shimo. Ulisikia ombi langu: “Usikizibie masikio yako kilio changu nikuombapo msaada.” Ulikuja karibu nilipokuita, nawe ukasema, “Usiogope.” Ee Bwana, ulichukua shauri langu, ukaukomboa uhai wangu. Umeona, Ee BWANA, ubaya niliotendewa. Tetea shauri langu! Umeona kina cha kisasi chao, mashauri yao yote mabaya dhidi yangu. Ee BWANA, umesikia matukano yao, mashauri yao yote mabaya dhidi yangu: kile adui zangu wanachonongʼona na kunungʼunikia dhidi yangu mchana kutwa. Watazame! Wakiwa wameketi au wamesimama, wananidhihaki katika nyimbo zao. Uwalipe kile wanachostahili, Ee BWANA, kwa yale ambayo mikono yao imetenda. Weka pazia juu ya mioyo yao, laana yako na iwe juu yao! Wafuatilie katika hasira na uwaangamize kutoka chini ya mbingu za BWANA.