Yobu 38:39-41
Yobu 38:39-41 Biblia Habari Njema (BHN)
“Je, waweza kumwindia simba mawindo yake au kuishibisha hamu ya wana simba; wanapojificha mapangoni mwao, au kulala mafichoni wakiotea? Ni nani awapaye kunguru chakula chao, makinda yao yanaponililia mimi Mungu, na kurukaruka huku na huko kwa njaa?
Yobu 38:39-41 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Je! Utamwindia simba mke mawindo? Au utashibisha njaa ya simba wachanga, Waoteapo mapangoni mwao, Wakaapo mafichoni wapate kuvizia? Ni nani anayempatia kunguru chakula, Makinda yake wanapomlilia Mungu, Na kutangatanga kwa kutindikiwa na chakula?
Yobu 38:39-41 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Je! Utamwindia simba mke mawindo? Au utashibisha njaa ya simba wachanga, Waoteapo mapangoni mwao, Wakaapo mafichoni wapate kuvizia? Ni nani anayempatia kunguru chakula, Makinda yake wanapomlilia Mungu, Na kutanga-tanga kwa kutindikiwa na chakula?
Yobu 38:39-41 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
“Je, utamwindia simba jike mawindo, na kuwashibisha simba wenye njaa wakati wao wamejikunyata mapangoni mwao, au wakivizia kichakani? Ni nani ampaye kunguru chakula wakati makinda yake yanamlilia Mungu, yakizungukazunguka kwa ajili ya kukosa chakula?