Yobu 36:16-26
Yobu 36:16-26 Biblia Habari Njema (BHN)
Mungu alikuvuta akakutoa taabuni, akakuweka mahali pa wasaa pasipo shida, na mezani pako akakuandalia vinono. “Lakini sasa umehukumiwa kama mwovu, hukumu ya haki imekukumba. Jihadhari ghadhabu isije ikakufanya ukadhihaki, au ukubwa wa mali za kukukomboa ukakupotosha. Je, kilio chako kitafaa kukutoa taabuni, au nguvu zako zote zitakusaidia? Usitamani usiku uje, ambapo watu hufanywa watoweke walipo. Jihadhari! Usiuelekee uovu maana umepatiwa mateso kukuepusha na uovu. Kumbuka ukuu wa uwezo wa Mungu; nani awezaye kumfundisha kitu? Nani basi aliyeweza kumpangia njia yake, au awezaye kumwambia: ‘Umekosea?’ “Usisahau kuyasifu matendo yake; ambayo watu wameyashangilia. Watu wote wameona aliyofanya Mungu; binadamu huyaona kutoka mbali. Mungu ni mkuu mno hata hatuwezi kumjua; muda wa maisha yake hauchunguziki.
Yobu 36:16-26 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Naam, yeye angekuongoza utoke katika msiba Hata mahali penye nafasi, ambapo hapana msonge; Na kilichowekwa mezani pako kingejaa mafuta. Lakini umejaa hukumu ya waovu; Hukumu na haki hukushika. Basi ujitunze, isije hasira ikakuvuta hata ukafanya mzaha; Wala usikubali ukuu wa ukombozi ukugeuze. Je! Mali yako yatatosha, hata usiwe katika taabu, Au uwezo wote wa nguvu zako? Usiutamani usiku, Wakati watu wakatwapo katika mahali pao. Jitunze, usiutazame uovu; Kwani umeuchagua huo zaidi ya taabu. Tazama, Mungu hutenda makuu kwa uweza wake; Ni nani afundishaye kama yeye? Ni nani aliyemwagiza njia yake? Au ni nani awezaye kusema, Wewe umetenda yasiyo haki? Kumbuka kuitukuza kazi yake, Watu waliyoiimbia. Wanadamu wote wameitazama; Watu huiangalia kwa mbali Tazama, Mungu ni mkuu, nasi hatumjui; Hesabu ya miaka yake haitafutiki.
Yobu 36:16-26 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Naam, yeye angekuongoza utoke katika msiba Hata mahali penye nafasi, ambapo hapana kizuizi; Na kilichowekwa mezani pako kingejaa mafuta. Lakini umejaa hukumu ya waovu; Hukumu na haki hukushika. Basi ujitunze, isije hasira ikakuvuta hata ukafanya mzaha; Wala usikubali ukuu wa ukombozi ukugeuze. Je! Mali yako itatosha, hata usiwe katika taabu, Au uwezo wote wa nguvu zako? Usiutamani usiku, Wakati watu wakatwapo katika mahali pao. Jitunze, usiutazame uovu; Kwani umeuchagua huo zaidi ya taabu. Tazama, Mungu hutenda makuu kwa uweza wake; Ni nani afundishaye kama yeye? Ni nani aliyemwagiza njia yake? Au ni nani awezaye kusema, Wewe umetenda yasiyo haki? Kumbuka kuitukuza kazi yake, Watu waliyoiimbia. Wanadamu wote wameitazama; Watu huiangalia kwa mbali. Tazama, Mungu ni mkuu, nasi hatumjui; Hesabu ya miaka yake haichunguziki.
Yobu 36:16-26 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
“Yeye anakubembeleza utoke katika mataya ya dhiki, ili kukuweka mahali palipo na nafasi mbali na kizuizi, hadi kwenye meza yako ya faraja iliyojaa vyakula vizuri. Lakini sasa umelemewa na hukumu kwa ajili ya uovu; hukumu na haki vimekukamata. Uwe mwangalifu ili yeyote asikushawishi kwa utajiri; usipotoshwe kwa fungu kubwa la rushwa. Je, utajiri wako hata nguvu zako nyingi vinaweza kukusaidia usiingie kwenye dhiki? Usiutamani usiku uje, ili uwaburute watu mbali na nyumba zao. Jihadhari usigeukie uovu, ambao unaupenda zaidi kuliko mateso. “Mungu ametukuzwa katika nguvu zake. Ni nani aliye mwalimu kama yeye? Ni nani aliyemwelekeza katika njia zake, au kumwambia, ‘Wewe umetenda yasiyo sawa’? Kumbuka kuzitukuza kazi zake, ambazo watu wamezisifu katika wimbo. Wanadamu wote wameiona; watu wanaikazia macho kwa mbali. Tazama jinsi Mungu alivyo mkuu, kupita ufahamu wetu! Hesabu ya miaka yake haitafutiki.