Yobu 34:1-15
Yobu 34:1-15 Biblia Habari Njema (BHN)
Kisha Elihu akaendelea kusema: “Sikilizeni maneno yangu enyi wenye hekima, nitegeeni masikio yenu, nyinyi wenye ujuzi. Sikio huyapima maneno, kama vile ulimi uonjavyo chakula. Basi, na tuchague lililo sawa, tuamue miongoni mwetu lililo jema. Basi, Yobu ametamka: ‘Mimi Yobu sina hatia, Mungu ameniondolea haki yangu. Ingawa sina hatia naonekana kuwa mwongo; kidonda changu hakiponyeki ingawa sina kosa.’ Ni nani aliye kama Yobu ambaye kwake ubaradhuli ni kama kunywa maji? Huandamana na watenda maovu hutembea na watu waovu. Maana amesema, ‘Mtu hapati faida yoyote, kujisumbua kumpendeza Mungu.’ “Kwa hiyo nisikilizeni, enyi wenye ujuzi. Mungu kamwe hawezi kufanya uovu; Mungu Mwenye Nguvu hawezi kufanya kosa. Mungu atamlipa mtu kadiri ya matendo yake, atamlipiza kulingana na mwenendo wake. Ni ukweli mtupu: Mungu hafanyi ovu; Mungu Mwenye Nguvu kamwe hapotoshi haki. Je, kuna aliyemkabidhi mamlaka juu ya dunia? Uwezo wake juu ya ulimwengu ni wake peke yake. Kama Mungu angejifikiria tu yeye mwenyewe, akiondoa pumzi yake ya uhai duniani, viumbe vyote vingeangamia kabisa, naye binadamu angerudi mavumbini.
Yobu 34:1-15 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Tena Elihu akajibu na kusema, Sikilizeni maneno yangu, enyi wenye hekima; Tegeni masikio kwangu, ninyi mlio na maarifa. Kwa kuwa sikio huyajaribu maneno, Kama vile kaakaa lionjavyo chakula. Na tujichagulie yaliyo ya uelekevu; Na tujue wenyewe yaliyo mema. Kwani Ayubu amesema, Mimi ni mwenye haki, Naye Mungu ameniondolea haki yangu; Nijapokuwa mwenye haki, nimehesabiwa kuwa mwongo; Jeraha langu haliponyeki, nijapokuwa sina makosa. Je! Ni mtu gani mfano wa Ayubu, Anywaye mzaha kama maji? Atembeaye na hao watendao uovu, Na kwenda pamoja na watu wabaya. Kwa kuwa amenena, Haimfai mtu lolote Kujifurahisha na Mungu. Kwa hiyo nisikilizeni, enyi wenye fahamu; Mungu asidhaniwe kutenda udhalimu; Wala Mwenyezi kufanya uovu. Kwani atamlipa binadamu kwa kazi yake, Naye atamfanya kila mtu kuona kulingana na njia zake. Naam, hakika, Mungu hatatenda mabaya, Wala Mwenyezi hatapotosha hukumu. Ni nani aliyemwagiza kuiangalia dunia? Au ni nani aliyemwekea ulimwengu huu wote? Kama akimwekea mtu moyo wake, Akijikusanyia roho yake na pumzi zake; Wenye mwili wote wangeangamia pamoja, Nao wanadamu watarejea tena kuwa mavumbi.
Yobu 34:1-15 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Tena Elihu akajibu na kusema, Sikilizeni maneno yangu, enyi wenye hekima; Tegeni masikio kwangu, ninyi mlio na maarifa. Kwa kuwa sikio huyajaribu maneno, Kama vile kaakaa lionjavyo chakula. Na tujichagulie yaliyo ya uelekevu; Na tujue wenyewe yaliyo mema. Kwani Ayubu amesema, Mimi ni mwenye haki, Naye Mungu ameniondolea haki yangu; Nijapokuwa mwenye haki, nimehesabiwa kuwa mwongo; Jeraha yangu haiponyeki, nijapokuwa sina makosa. Je! Ni mtu gani mfano wa Ayubu, Anywaye mzaha kama maji? Atembeaye na hao watendao uovu, Na kwenda pamoja na watu wabaya. Kwa kuwa amenena, Haimfai mtu lo lote Kujifurahisha na Mungu. Kwa hiyo nisikilizeni, enyi wenye fahamu; Mungu asidhaniwe kutenda udhalimu; Wala Mwenyezi kufanya uovu. Kwani atamlipa binadamu kwa kazi yake, Naye atamfanya kila mtu kuona sawasawa na njia zake Naam, hakika, Mungu hatatenda mabaya, Wala Mwenyezi hatapotosha hukumu. Ni nani aliyemwagiza kuiangalia dunia? Au ni nani aliyemwekea ulimwengu huu wote? Kama akimwekea mtu moyo wake, Akijikusanyia roho yake na pumzi zake; Wenye mwili wote wataangamia pamoja, Nao wanadamu watarejea tena kuwa mavumbi.
Yobu 34:1-15 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Kisha Elihu akasema: “Sikieni maneno yangu, enyi watu wenye hekima; nisikilizeni mimi, ninyi watu wenye maarifa. Kwa kuwa sikio huyajaribu maneno kama vile ulimi uonjavyo chakula. Tujichagulie wenyewe yaliyo sawa, nasi tujifunze pamoja yaliyo mema. “Ayubu anasema, ‘Mimi sina hatia, lakini Mungu ameninyima haki yangu. Ingawa niko sawa, ninaonekana mwongo; nami ingawa sina kosa, kidonda changu hakiponi.’ Ni mtu gani aliye kama Ayubu, anywaye dharau kama maji? Ashirikianaye na watenda mabaya na kuchangamana na watu waovu. Kwa kuwa anasema, ‘Haimfaidi mwanadamu kitu chochote anapojitahidi kumpendeza Mungu.’ “Hivyo nisikilizeni mimi, ninyi watu wenye ufahamu. Kamwe Mungu hatendi uovu, Mwenyezi hafanyi kosa. Humlipa mwanadamu kwa ajili ya lile alilotenda; huleta juu yake kile ambacho matendo yake yanastahili. Ni jambo lisiloweza kufikiriwa kwamba Mungu angefanya makosa, kwamba Mwenyezi angepotosha hukumu. Je, ni nani aliyemtawaza juu ya dunia? Ni nani aliyemweka kuwa mwangalizi wa ulimwengu wote? Kama lilikuwa kusudi la Mungu, naye akaiondoa Roho yake na pumzi yake, wanadamu wote wangeliangamia kwa pamoja, na mtu angerudi mavumbini.