Yobu 32:6-9
Yobu 32:6-9 Biblia Habari Njema (BHN)
Basi, Elihu mwana wa Barakeli, wa kabila la Buzi akaanza kusema: “Mimi ni kijana, nyinyi ni wazee zaidi; kwa hiyo niliogopa kuwaambieni mawazo yangu. Nilisema moyoni: ‘Waache wenye siku nyingi waseme, wenye miaka mingi wafundishe hekima.’ Lakini hiyo roho iliyomo ndani ya mtu, hiyo pumzi ya Mungu Mwenye Nguvu, ndio inayomwezesha mwanadamu kufahamu. Si lazima kuwa mzee ili uwe na hekima wala wazee siyo wenye kufahamu lililo sawa.
Yobu 32:6-9 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Basi Elihu mwana wa Barakeli, Mbuzi, akajibu, na kusema, Mimi ni kijana, na ninyi ni wazee sana; Kwa hiyo nilijizuia, nisithubutu kuwaonesha nionavyo. Nilisema, Yafaa siku ziseme, Na wingi wa miaka ufundishe hekima. Lakini hakika imo roho ndani ya mwanadamu, Na pumzi ya Mwenyezi ndiyo impayo ufahamu. Sio wakuu walio wenye hekima, Wala sio wazee watambuao haki.
Yobu 32:6-9 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Basi Elihu mwana wa Barakeli, Mbuzi, akajibu, na kusema, Mimi ni kijana, na ninyi ni wazee sana; Kwa hiyo nilijizuia, nisithubutu kuwaonyesha nionavyo. Nilisema, Yafaa siku ziseme, Na wingi wa miaka ufundishe hekima. Lakini imo roho ndani ya mwanadamu, Na pumzi za Mwenyezi huwapa akili. Sio wakuu walio wenye akili, Wala sio wazee watambuao hukumu.
Yobu 32:6-9 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Basi Elihu mwana wa Barakeli wa kabila la Buzi akasema: “Mimi ni mdogo kwa umri, nanyi ni wazee; ndiyo sababu niliogopa, sikuthubutu kuwaambia kile ninachojua. Nilifikiri, ‘Yafaa umri useme, nao wingi wa miaka ungefundisha hekima.’ Lakini ni Roho iliyoko ndani ya mwanadamu, pumzi ya Mwenyezi, ndiyo impayo yeye ufahamu. Sio wazee peke yao walio na hekima, sio wenye umri mkubwa peke yao wanaofahamu lililo sawa.