Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yobu 28:1-19

Yobu 28:1-19 Biblia Habari Njema (BHN)

“Hakika kuna machimbo ya fedha, na mahali ambako dhahabu husafishwa. Watu huchimba chuma ardhini, huyeyusha shaba kutoka mawe ya madini. Wachimba migodi huleta taa gizani, huchunguza vina vya ardhi na kuchimbua mawe yenye madini gizani. Binadamu huchimba mashimo mbali na makazi ya watu, mbali na watu mahali kusipofikika, wachimba madini huninginia wamefungwa kamba. Kutoka udongoni chakula hupatikana, lakini chini yake kila kitu huvurugwa kwa moto. Katika mawe yake ndimo vilimo vito vya rangi ya samawati na udongo wake una vumbi la dhahabu. “Njia za kwenda kwenye migodi hiyo hakuna ndege mla nyama azijuaye; na wala jicho la tai halijaiona. Wanyama waendao kwa madaha hawajazikanyaga wala simba hawajawahi kuzipitia. Binadamu huchimbua miamba migumu kabisa, huichimbua milima na kuiondolea mbali. Hupasua mifereji kati ya majabali, na jicho lake huona vito vya thamani. Huziba chemchemi zisitiririke, na kufichua vitu vilivyofichika. “Lakini hekima itapatikana wapi? Ni mahali gani panapopatikana maarifa? Hakuna mtu ajuaye thamani ya hekima, wala hekima haipatikani nchini mwa walio hai. Vilindi vyasema, ‘Hekima haimo kwetu,’ na bahari yasema, ‘Haiko kwangu.’ Hekima haiwezi kupatikana kwa dhahabu, wala kwa kupima kiasi kingi cha fedha. Haiwezi kupimwa kwa dhahabu ya Ofiri, wala kwa vito vya Sardoniki au vya rangi ya samawati, dhahabu au kioo havilingani nayo, wala haiwezi kubadilishwa na vito vya dhahabu safi. Hekima ina thamani kuliko matumbawe na marijani, thamani yake yashinda thamani ya lulu. Topazi ya Kushi haiwezi kulinganishwa nayo, wala haiwezi kupewa bei ya dhahabu safi.

Shirikisha
Soma Yobu 28

Yobu 28:1-19 Swahili Revised Union Version (SRUV)

Hakika kuna shimo wachimbako fedha, Na mahali wapatapo dhahabu waisafishayo. Chuma hufukuliwa katika ardhi, Na shaba huyeyushwa katika mawe. Binadamu hukomesha giza; Huyatafutatafuta hata katika maeneo ya mbali, Mawe ya madini katika giza, giza kuu. Hufukua shimo mbali na makao ya watu; Husahauliwa na nyayo zipitazo; Huning'inia mbali na watu, huyumbayumba huku na huko. Katika ardhi ndimo kitokeamo chakula; Na chini yake hupinduliwa kama kwa moto. Mawe yake ni mahali zipatikanapo yakuti; Nayo ina mchanga wa dhahabu. Njia ile hapana ndege mkali aijuaye, Wala jicho la tai halijaiona; Wanyama wakali wajivunao hawajaikanyaga, Wala simba mkali hajaipita. Huunyoshea mwamba wa gumegume mkono wake; Huipindua milima hata misingi yake. Hukata mifereji kati ya majabali; Na jicho lake huona kila kito cha thamani. Hufunga vijito visichuruzike; Na kitu kilichositirika hukifunua. Bali hekima itapatikana wapi? Na mahali pa ufahamu ni wapi? Mwanadamu hajui thamani yake, Wala haionekani katika nchi ya walio hai. Vilindi vyasema, Haimo ndani yangu; Na bahari yasema, Haiko kwangu. Haipatikani kwa dhahabu, Wala fedha haitapimwa iwe thamani yake. Haiwezi kutiwa thamani kwa dhahabu ya Ofiri, Wala kwa shohamu ya thamani nyingi, wala kwa yakuti samawi. Dhahabu na vioo haviwezi kulinganishwa nayo; Wala kubadili kwake hakutakuwa kwa vyombo vya dhahabu safi. Havitatajwa fedhaluka wala bilauri; Naam, kima cha hekima chapita marijani. Yakuti ya rangi ya manjano ya Kushi haitasawazishwa nayo, Wala haitatiwa kima kwa dhahabu safi.

Shirikisha
Soma Yobu 28

Yobu 28:1-19 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)

Hakika kuna shimo wachimbako fedha, Na mahali wapatapo dhahabu waisafishayo. Chuma hufukuliwa katika ardhi, Na shaba huyeyushwa katika mawe. Binadamu hukomesha giza; Huyatafuta-tafuta hata mpaka ulio mbali, Mawe ya giza kuu, giza tupu. Hufukua shimo mbali na makao ya watu; Husahauliwa na nyayo zipitazo; Huning’inia mbali na watu, huyumba-yumba huko na huko. Katika ardhi ndimo kitokeamo chakula; Na chini yake hupinduliwa kama kwa moto. Mawe yake ni mahali zipatikanapo yakuti; Nayo ina mchanga wa dhahabu. Njia ile hapana ndege mkali aijuaye, Wala jicho la tai halijaiona; Wanyama wakali wajivunao hawajaikanyaga, Wala simba mkali hajaipita. Huunyoshea mwamba wa gumegume mkono wake; Huipindua milima hata misingi yake. Hukata mifereji kati ya majabali; Na jicho lake huona kila kito cha thamani Hufunga vijito visichuruzike; Na kitu kilichostirika hukifunua. Bali hekima itapatikana wapi? Na mahali pa ufahamu ni wapi? Mwanadamu hajui thamani yake, Wala haionekani katika nchi ya walio hai. Vilindi vyasema, Haimo ndani yangu; Na bahari yasema, Haiko kwangu. Haipatikani kwa dhahabu, Wala fedha haitapimwa iwe thamani yake. Haiwezi kutiwa thamani kwa dhahabu ya Ofiri, Wala kwa shohamu ya thamani nyingi, wala kwa yakuti ya samawi. Dhahabu na vioo haviwezi kulinganishwa nayo; Wala kubadili kwake hakutakuwa kwa vyombo vya dhahabu safi. Havitatajwa fedhaluka wala bilauri; Naam, kima cha hekima chapita marijani. Yakuti ya rangi ya manjano ya Kushi haitasawazishwa nayo, Wala haitatiwa kima kwa dhahabu safi.

Shirikisha
Soma Yobu 28

Yobu 28:1-19 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)

“Kuna machimbo ya fedha, na mahali dhahabu isafishwapo. Chuma hupatikana ardhini, nayo shaba huyeyushwa kutoka mawe ya madini. Mwanadamu hukomesha giza; huyatafuta hadi sehemu iliyo mbali, kwa ajili ya kuchimbua mawe yenye madini katika giza jeusi sana. Huchimba shimo jembamba mbali na makao ya watu, mahali paliposahaulika na nyayo za wanadamu; mbali na wanadamu huningʼinia na kupembea kwa kamba. Ardhi, ambako chakula hutoka, chini hugeuzwa kwa moto; yakuti samawi hutoka katika miamba yake, nalo vumbi lake lina vipande vya dhahabu. Hakuna ndege awindaye aijuaye njia ile iliyofichika, wala hakuna jicho la mwewe lililoiona. Wanyama wa porini wanaotamba hawajawahi kupakanyaga, wala simba azungukaye huko. Mikono ya mwanadamu hushambulia miamba migumu sana, na kuiacha wazi mizizi ya milima. Hutoboa shimo refu la kupenya chini kwa chini kwenye miamba; macho yake huona hazina zake zote. Hutafuta vyanzo vya mito na kuvileta vitu vilivyofichika katika nuru. “Lakini hekima inaweza kupatikana wapi? Ufahamu unakaa wapi? Mwanadamu hatambui thamani yake; haiwezi kupatikana katika nchi ya walio hai. Kilindi husema, ‘Haiko ndani yangu’; bahari nayo husema, ‘Haiko pamoja nami.’ Haiwezi kununuliwa kwa dhahabu safi kuliko zote, wala thamani yake haiwezi kupimwa kwa fedha. Haiwezi kununuliwa kwa dhahabu ya Ofiri, kwa shohamu ya thamani kubwa au yakuti samawi ya thamani kubwa. Dhahabu wala mawe maangavu haviwezi kulinganishwa nayo, wala haiwezi hubadilishwa na vito vya dhahabu. Marijani na yaspi hazistahili kutajwa; thamani ya hekima ni zaidi ya akiki nyekundu. Yakuti manjano ipatikanayo Kushi haiwezi kulinganishwa nayo, wala haiwezi kununuliwa kwa dhahabu safi.

Shirikisha
Soma Yobu 28