Yobu 26:5-14
Yobu 26:5-14 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Hao waliokufa watetemesha Chini ya maji na hao wakaamo humo. Kaburi li wazi mbele yake, Uharibifu nao hauna kifuniko. Yeye hutandaza kaskazi juu ya nafasi isiyo na kitu, Na kuutundika ulimwengu pasipo kitu. Huyafunga maji ndani ya mawingu yake mazito; Na hilo wingu halipasuki chini yake. Husitiri uso wa kiti chake cha enzi, Na kulitandaza wingu lake juu yake. Amepiga duara kuwa ni mpaka juu ya uso wa maji, Hata hapo mwanga na giza vinapopakana. Nguzo za mbingu zatetemeka, Na kustaajabu kwa kukemea kwake. Huichafua bahari kwa uwezo wake, Na kumtema Rahabu kwa akili zake. Hizo mbingu hupambwa kwa roho yake; Mkono wake umemchoma nyoka aendaye mbio. Tazama, hivi ni viunga tu vya njia zake; Na jinsi yalivyo madogo manong'ono tusikiayo katika habari zake! Lakini ngurumo za uweza wake ni nani awezaye kuzielewa?
Yobu 26:5-14 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Hao waliokufa watetema Chini ya maji na hao wayakaao. Kaburi li wazi mbele yake, Uharibifu nao hauna kifuniko. Yeye hutandaza kaskazi juu ya nafasi isiyo na kitu, Na kuutundika ulimwengu pasipo kitu. Huyafunga maji ndani ya mawingu yake mazito; Na hilo wingu halipasuki chini yake. Husitiri uso wa kiti chake cha enzi, Na kulitandaza wingu lake juu yake. Amepiga duara kuwa ni mpaka juu ya uso wa maji, Hata hapo mwanga na giza vinapopakana. Nguzo za mbingu zatetemeka, Na kustaajabu kwa kukemea kwake. Huichafua bahari kwa uwezo wake, Na kumtema Rahabu kwa akili zake. Hizo mbingu hupambwa kwa roho yake; Mkono wake umemchoma nyoka aendaye mbio. Tazama, hivi ni viunga tu vya njia zake; Na jinsi yalivyo madogo manong’ono tusikiayo katika habari zake! Lakini ngurumo za uweza wake ni nani awezaye kuelewa nazo?
Yobu 26:5-14 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
“Wafu wako katika maumivu makuu, wale walio chini ya maji na wale waishio ndani yake. Mauti iko wazi mbele za Mungu; Uharibifu haukufunikwa. Hutandaza anga la kaskazini mahali patupu; naye huiningʼiniza dunia mahali pasipo na kitu. Huyafungia maji kwenye mawingu yake, hata hivyo mawingu hayapasuki kwa uzito wake. Huufunika uso wa mwezi mpevu, akitandaza mawingu juu yake. Amechora mstari wa upeo juu ya uso wa maji, ameweka mpaka wa nuru na giza. Nguzo za mbingu nazo zatetemeka, zinatishika anapozikemea. Kwa nguvu zake aliisukasuka bahari; kwa hekima yake alimkata Rahabu vipande vipande. Aliisafisha anga kwa pumzi yake; kwa mkono wake alimchoma joka aendaye mbio. Haya ni mambo madogo tu katika matendo yake; tazama jinsi ulivyo mdogo mnongʼono tunaousikia kumhusu! Ni nani basi awezaye kuelewa ngurumo za nguvu zake?”
Yobu 26:5-14 Biblia Habari Njema (BHN)
“Mizimu huko chini yatetemeka, maji ya chini na wakazi wake yaogopa. Kuzimu kuko wazi kabisa mbele ya Mungu. Abadoni haina kifuniko chochote. Mungu hutandaza kaskazini mahali patupu, na hutundika dunia mahali pasipo na kitu, huyafunga maji mawinguni yawe mazito, nayo mawingu hayapasuki kwa uzito wake. Huufunika uso wa mwezi na kutandaza juu yake wingu. Amechora duara juu ya uso wa bahari, penye mpaka kati ya mwanga na giza. Mungu akitoa sauti ya kukemea, nguzo za mbingu hutetemeka na kustaajabu. Kwa nguvu zake aliituliza bahari; kwa maarifa yake alimwangamiza dude Rahabu. Kwa pumzi yake aliisafisha anga; mkono wake ulilichoma joka lirukalo. Yamkini haya ni machache tu ya matendo yake, ni minongono tu tunayosikia juu yake. Nani awezaye kujua ukuu wa nguvu yake?”