Yobu 11:6-10
Yobu 11:6-10 Biblia Habari Njema (BHN)
Angekueleza siri za hekima, maana yeye ni mwingi wa maarifa. Jua kwamba Mungu hakuhesabu makosa yako yote. “Je, unaweza kugundua siri zake Mungu na kujua ukomo wake yeye Mungu mwenye nguvu? Ukuu wake wapita mbingu, wewe waweza nini? Kimo chake chapita Kuzimu, wewe waweza kujua nini? Ukuu huo wapita marefu ya dunia, wapita mapana ya bahari. Kama Mungu akipita, akamfunga mtu na kumhukumu, nani awezaye kumzuia?
Yobu 11:6-10 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Tena akuoneshe hizo siri za hekima, Ya kuwa hufanikiwa katika kuyatimiza makusudi yake! Ujue basi ya kuwa Mungu akuachilia katika uovu wako. Je! Wewe waweza kuuvumbua ukuu wa Mungu? Waweza kuufikia upeo wa huyo Mwenyezi? Ni juu mno kama mbingu; waweza kufanya nini wewe? Ni wenye kina kuliko kuzimuni; waweza kujua nini wewe? Cheo chake ni kirefu kuliko dunia, Ni kipana zaidi ya bahari. Yeye akipita, na kufunga watu, Na kuwaita hukumuni, ni nani basi awezaye kumzuia?
Yobu 11:6-10 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Tena akuonyeshe hizo siri za hekima, Ya kuwa hufanikiwa katika kuyatimiza makusudi yake! Ujue basi ya kuwa Mungu akuachilia katika uovu wako. Je! Wewe waweza kuuvumbua ukuu wa Mungu? Waweza kuufikilia upeo wa huyo Mwenyezi? Ni juu mno kama mbingu; waweza kufanya nini wewe? Ni wenye kina kuliko kuzimuni; waweza kujua nini wewe? Cheo chake ni kirefu kuliko dunia, Ni kipana zaidi ya bahari. Yeye akipita, na kufunga watu, Na kuwaita hukumuni, ni nani basi awezaye kumzuia?
Yobu 11:6-10 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
naye akufunulie siri za hekima, kwa kuwa hekima ya kweli ina pande mbili. Ujue hili: Mungu amesahau hata baadhi ya dhambi zako. “Je, waweza kujua siri za Mungu? Je, waweza kuyachunguza mambo yote kumhusu Mwenyezi? Ni juu mno kuliko mbingu: waweza kufanya nini? Kina chake ni kirefu kuliko kuzimu: wewe waweza kujua nini? Kipimo chake ni kirefu kuliko dunia, nacho ni kipana kuliko bahari. “Kama akija na kukufunga gerezani, na kuitisha mahakama, ni nani awezaye kumpinga?