Yeremia 51:57-58
Yeremia 51:57-58 Biblia Habari Njema (BHN)
Nitawalewesha wakuu na wenye hekima wake, watawala wake, madiwani na askari wake; watalala usingizi wa milele wasiinuke tena. Nasema mimi mfalme ambaye jina langu ni Mwenyezi-Mungu wa Majeshi. “Mimi Mwenyezi-Mungu wa Majeshi nasema: Ukuta mpana wa Babuloni utabomolewa mpaka chini, na malango yake marefu yatateketezwa kwa moto. Watu wanafanya juhudi za bure, mataifa yanajichosha maana mwisho wao ni motoni!”
Yeremia 51:57-58 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Nami nitawalevya wakuu wake, na watu wake wenye hekima, watawala wake, na makamanda wake, na mashujaa wake; nao watalala usingizi wa milele, wasiamke, asema Mfalme, BWANA wa majeshi, ambaye jina lake ni BWANA. BWANA wa majeshi asema hivi, Kuta pana za Babeli zitabomolewa kabisa, na malango yake marefu yatateketezwa; nao watu watajitaabisha kwa ubatili, na mataifa kwa moto; nao watachoka.
Yeremia 51:57-58 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Nami nitawalevya wakuu wake, na watu wake wenye hekima, maliwali wake, na maakida wake, na mashujaa wake; nao watalala usingizi wa milele, wasiamke, asema Mfalme, BWANA wa majeshi, ambaye jina lake ni BWANA. BWANA wa majeshi asema hivi, Kuta pana za Babeli zitabomolewa kabisa, na malango yake marefu yatateketezwa; nao watu watajitaabisha kwa ubatili, na mataifa kwa moto; nao watachoka.
Yeremia 51:57-58 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Nitawafanya maafisa wake na wenye busara walewe, watawala wao, maafisa, pamoja na wapiganaji wao; watalala milele na hawataamka,” asema Mfalme, ambaye jina lake ni BWANA Mwenye Nguvu Zote. Hili ndilo BWANA Mwenye Nguvu Zote asemalo: “Ukuta mnene wa Babeli utasawazishwa, na malango yaliyoinuka yatateketezwa kwa moto; mataifa yanajichosha bure, taabu ya mataifa ni nishati tu ya miali ya moto.”