Yeremia 51:51-53
Yeremia 51:51-53 Biblia Habari Njema (BHN)
Mnasema: ‘Tumeaibishwa na kufadhaishwa; aibu imezifunika nyuso zetu, kwa sababu wageni wameingia katika sehemu takatifu za nyumba ya Mwenyezi-Mungu.’ “Kwa hiyo, wakati unakuja, nasema mimi Mwenyezi-Mungu, ambapo nitaviadhibu vinyago vya Babuloni, na majeruhi watapiga kite katika nchi yake yote. Ingawa Babuloni atapanda mpaka mbinguni, na kuziimarisha ngome zake ndefu, waangamizi watakuja kutoka kwangu kumvamia. 2Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.
Yeremia 51:51-53 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
“Tumetahayari, kwa maana tumetukanwa na aibu imefunika nyuso zetu, kwa sababu wageni wameingia mahali patakatifu pa nyumba ya BWANA.” “Lakini siku zinakuja,” asema BWANA, “nitakapoadhibu sanamu zake, na katika nchi yake yote waliojeruhiwa watalia kwa maumivu makali. Hata kama Babeli ikifika angani na kuziimarisha ngome zake ndefu, nitatuma waharabu dhidi yake,” asema BWANA.
Yeremia 51:51-53 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Twaona haya kwa kuwa tumesikia shutuma; Fedheha imetufunika nyuso zetu; Kwa sababu wageni wamepaingia Patakatifu pa nyumba ya BWANA. Kwa sababu hiyo siku zinakuja, asema BWANA, nitakapozihukumu sanamu zake; na katika nchi yake yote waliojeruhiwa wataomboleza. Babeli ujapopanda mbinguni, na ujapopafanya mahali pa juu penye nguvu zake kuwa ngome, hata hivyo toka kwangu wenye kuangamiza watamwendea, asema BWANA.
Yeremia 51:51-53 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Twaona haya kwa kuwa tumesikia mashutumu; Fedheha imetufunikiza nyuso zetu; Kwa sababu wageni wamepaingia Patakatifu pa nyumba ya BWANA. Kwa sababu hiyo siku zinakuja, asema BWANA, nitakapozihukumu sanamu zake; na katika nchi yake yote waliojeruhiwa wataugua. Babeli ujapopanda mbinguni, na ujapopafanya mahali pa juu penye nguvu zake kuwa ngome, hata hivyo toka kwangu wenye kuangamiza watamwendea, asema BWANA.