Yeremia 51:44-45
Yeremia 51:44-45 Biblia Habari Njema (BHN)
Nitamwadhibu mungu Beli huko Babuloni, nitamfanya akitoe alichokimeza. Mataifa hayatamiminika tena kumwendea. Ukuta wa Babuloni umebomoka. “Tokeni humo enyi watu wangu! Kila mtu na ayasalimishe maisha yake, kutoka hasira kali ya Mwenyezi-Mungu.
Yeremia 51:44-45 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Nitamwadhibu Beli katika Babeli, na kumfanya atapike kile alichokimeza. Mataifa hayatamiminika tena kwake. Nao ukuta wa Babeli utaanguka. “Tokeni ndani yake, enyi watu wangu! Okoeni maisha yenu! Ikimbieni hasira kali ya BWANA.
Yeremia 51:44-45 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Nami nitafanya hukumu juu ya Beli katika Babeli, nami nitavitoa katika kinywa chake alivyovimeza; wala mataifa hawatamwendea tena; naam, ukuta wa Babeli utaanguka. Enyi watu wangu; tokeni katikati yake, mkajiokoe nafsi zenu kutoka kwa hasira kali ya BWANA, kila mmoja wenu.
Yeremia 51:44-45 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Nami nitafanya hukumu juu ya Beli katika Babeli, nami nitavitoa katika kinywa chake alivyovimeza; wala mataifa hawatamwendea tena; naam, ukuta wa Babeli utaanguka. Enyi watu wangu; tokeni katikati yake, mkajiokoe nafsi zenu na hasira kali ya BWANA, kila mmoja wenu.