Yeremia 4:13-14
Yeremia 4:13-14 Biblia Habari Njema (BHN)
Tazama! Adui anakuja kama mawingu. Magari yake ya vita ni kama kimbunga, na farasi wake waenda kasi kuliko tai. Ole wetu! Tumeangamia! Yerusalemu, yasafishe maovu moyoni mwako, ili upate kuokolewa. Mpaka lini utaendelea kuwaza maovu?
Yeremia 4:13-14 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Tazama atapanda juu kama mawingu, na magari yake ya vita yatakuwa kama kisulisuli; farasi wake ni wepesi kuliko tai. Ole wetu, kwa sababu tumeharibika. Ee Yerusalemu, jioshe moyo wako usiwe na uovu, upate kuokoka. Mawazo yako mabaya yatakaa ndani yako hata lini?
Yeremia 4:13-14 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Tazama atapanda juu kama mawingu, na magari yake ya vita yatakuwa kama kisulisuli; farasi zake ni wepesi kuliko tai. Ole wetu, kwa sababu tumeharibika. Ee Yerusalemu, jioshe moyo wako usiwe na uovu, upate kuokoka. Mawazo yako mabaya yatakaa ndani yako hata lini?
Yeremia 4:13-14 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Tazama! Anakuja kama mawingu, magari yake yanakuja kama upepo wa kisulisuli, farasi wake wana mbio kuliko tai. Ole wetu! Tunaangamia! Ee Yerusalemu, usafishe uovu kutoka moyoni mwako na uokolewe. Utaendelea kuficha mawazo mapotovu mpaka lini?