Yeremia 19:15
Yeremia 19:15 Biblia Habari Njema (BHN)
“Mwenyezi-Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi: Tazama, mimi nitauletea mji huu na vijiji vyote vilivyo jirani maafa yote niliyoutangazia, kwa sababu wakazi wake ni wakaidi na wamekataa kusikia maneno yangu.”
Yeremia 19:15 Swahili Revised Union Version (SRUV)
BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Tazama, nitaleta juu ya mji huu, na juu ya vijiji vyake vyote, mabaya yote niliyoyanena juu yake; kwa sababu wamefanya shingo zao kuwa ngumu, wasiyasikie maneno yangu.
Yeremia 19:15 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Tazama, nitaleta juu ya mji huu, na juu ya vijiji vyake vyote, mabaya yote niliyoyanena juu yake; kwa sababu wamefanya shingo zao kuwa ngumu, kusudi wasiyasikie maneno yangu.
Yeremia 19:15 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
“Hili ndilo BWANA Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo: ‘Sikilizeni! Nitaleta juu ya mji huu pamoja na vijiji vinavyouzunguka kila maafa niliyosema dhidi yake, kwa sababu wamekuwa na shingo ngumu, na hawakuyasikiliza maneno yangu.’ ”