Yeremia 19:14-15
Yeremia 19:14-15 Biblia Habari Njema (BHN)
Baada ya hayo, Yeremia aliondoka Tofethi, mahali ambako Mwenyezi-Mungu alimtuma aende kutoa unabii, akaenda na kusimama katika ukumbi wa nyumba ya Mwenyezi-Mungu, akawatangazia watu wote akisema: “Mwenyezi-Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi: Tazama, mimi nitauletea mji huu na vijiji vyote vilivyo jirani maafa yote niliyoutangazia, kwa sababu wakazi wake ni wakaidi na wamekataa kusikia maneno yangu.”
Yeremia 19:14-15 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kisha Yeremia akatoka huko Tofethi, huko ambako BWANA alimtuma atoe unabii; naye akasimama katika ua wa nyumba ya BWANA, akawaambia watu wote, BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Tazama, nitaleta juu ya mji huu, na juu ya vijiji vyake vyote, mabaya yote niliyoyanena juu yake; kwa sababu wamefanya shingo zao kuwa ngumu, wasiyasikie maneno yangu.
Yeremia 19:14-15 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kisha Yeremia akatoka huko Tofethi, huko ambako BWANA alimtuma atoe unabii; naye akasimama katika ua wa nyumba ya BWANA, akawaambia watu wote, BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Tazama, nitaleta juu ya mji huu, na juu ya vijiji vyake vyote, mabaya yote niliyoyanena juu yake; kwa sababu wamefanya shingo zao kuwa ngumu, kusudi wasiyasikie maneno yangu.
Yeremia 19:14-15 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Kisha Yeremia akarudi kutoka Tofethi, mahali ambapo BWANA alikuwa amemtuma kutoa unabii, akasimama katika ua wa Hekalu la BWANA na kuwaambia watu wote, “Hili ndilo BWANA Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo: ‘Sikilizeni! Nitaleta juu ya mji huu pamoja na vijiji vinavyouzunguka kila maafa niliyosema dhidi yake, kwa sababu wamekuwa na shingo ngumu, na hawakuyasikiliza maneno yangu.’ ”