Yeremia 18:9-10
Yeremia 18:9-10 Biblia Habari Njema (BHN)
Hali kadhalika, wakati wowote nikitoa tamko kuhusu taifa au ufalme kwamba nitalijenga na kulistawisha, kisha taifa hilo likafanya uovu mbele yangu na kukataa kunitii, basi, mimi nitaacha kulitendea mema hayo niliyokusudia kulitendea.
Yeremia 18:9-10 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Na wakati wowote nitakapotoa habari za taifa, na habari za ufalme, kuujenga na kuupanda, ikiwa watatenda maovu mbele za macho yangu, wasiitii sauti yangu, basi nitaghairi, nisitende mema yale niliyoazimia kuwatendea.
Yeremia 18:9-10 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Na wakati wo wote nitakapotoa habari za taifa, na habari za ufalme, kuujenga na kuupanda, ikiwa watatenda maovu mbele za macho yangu, wasiitii sauti yangu, basi nitaghairi, nisitende mema yale niliyoazimia kuwatendea.