Yeremia 13:15-16
Yeremia 13:15-16 Biblia Habari Njema (BHN)
Enyi Waisraeli, sikilizeni kwa makini, msiwe na majivuno maana Mwenyezi-Mungu anasema nanyi. Mtukuzeni Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, kabla hajawaletea giza, nanyi mkajikwaa miguu kwenye milima ya giza. Nyinyi mnatazamia mwanga, lakini anaugeuza kuwa utusitusi na kuufanya kuwa giza nene.
Yeremia 13:15-16 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Sikieni na mzingatie, msiwe na kiburi, kwa kuwa BWANA amenena. Mpeni utukufu BWANA Mungu wenu, kabla hajaleta giza, kabla miguu yenu haijajikwaa juu ya vilima vitakavyotiwa giza. Mlitarajia nuru, lakini ataifanya kuwa giza nene na kuibadili kuwa huzuni kubwa.
Yeremia 13:15-16 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Sikilizeni ninyi, kategeni masikio yenu; msifanye kiburi; maana BWANA amenena. Mtukuzeni BWANA, Mungu wenu, kabla hajaleta giza, na kabla miguu yenu haijakwaa juu ya milima yenye giza; na wakati mnapoitazamia nuru, kabla hajaigeuza kuwa kivuli cha mauti, na giza nene.
Yeremia 13:15-16 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)