Yeremia 10:17-25
Yeremia 10:17-25 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Kusanyeni mali na vitu vyenu mwondoke nchi hii, enyi mnaoishi katika hali ya kuzingirwa na jeshi. Kwa kuwa hili ndilo asemalo BWANA: “Wakati huu, nitawatupa nje kwa nguvu wote waishio katika nchi hii; nitawataabisha ili waweze kutekwa.” Ole wangu mimi kwa ajili ya kuumia kwangu! Jeraha langu ni kubwa! Lakini nilisema, “Kweli hii ni adhabu yangu, nami sharti niistahimili.” Hema langu limeangamizwa; kamba zake zote zimekatwa. Wana wangu wametekwa na hawapo tena; hakuna hata mmoja aliyebaki wa kusimamisha hema langu wala wa kusimamisha kibanda changu. Wachungaji hawana akili wala hawamuulizi BWANA, hivyo hawastawi na kundi lao lote la kondoo limetawanyika. Sikilizeni! Taarifa inakuja: ghasia kubwa kutoka nchi ya kaskazini! Hii itafanya miji ya Yuda ukiwa, makao ya mbweha. Ninajua, Ee BWANA, kwamba maisha ya mwanadamu si yake mwenyewe; hawezi kuziongoza hatua zake mwenyewe. Unirudi, Ee BWANA, lakini kwa kipimo cha haki: si katika hasira yako, usije ukaniangamiza. Umwage ghadhabu yako juu ya mataifa wasiokujua wewe, juu ya mataifa wasioliitia jina lako. Kwa kuwa wamemwangamiza Yakobo; wamemwangamiza kabisa na kuiharibu nchi yake.
Yeremia 10:17-25 Biblia Habari Njema (BHN)
Kusanyeni vitu vyenu enyi watu mliozingirwa. Maana Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Wakati huo nitawatupa nje ya nchi hii, nitawataabisha asibaki mtu yeyote.” Ole wangu mimi Yerusalemu maana nimejeruhiwa! Jeraha langu ni baya sana! Lakini nilisema: “Hakika haya ni mateso, na sina budi kuyavumilia.” Lakini hema langu limebomolewa, kamba zake zote zimekatika; watoto wangu wameniacha, na kwenda zao, wala hawapo tena; hakuna wa kunisimikia tena hema langu, wala wa kunitundikia mapazia yangu. Nami Yeremia nikasema: Wachungaji wamekuwa wajinga, hawakuomba shauri kwa Mwenyezi-Mungu; kwa sababu hiyo, hawakufanikiwa, na kondoo wao wote wametawanyika. Sikilizeni sauti! Habari zinatufikia. Kuna kishindo kutoka kaskazini. Taifa kutoka kaskazini linakuja, kuifanya miji ya Yuda kuwa jangwa ambamo kutakuwa na mapango ya mbweha! Najua, ee Mwenyezi-Mungu, binadamu hana uwezo na maisha yake; hakuna mtu awezaye kuyaongoza maisha yake. Utukosoe, ee Mwenyezi-Mungu, lakini si kwa ghadhabu, wala kwa hasira yako, tusije tukaangamia. Imwage hasira yako juu ya mataifa yasiyokuabudu, na juu ya watu ambao hawakutambui. Maana, wamewaua wazawa wa Yakobo; wamewaua na kuwaangamiza kabisa, na nchi yao wameiacha magofu.
Yeremia 10:17-25 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Haya! Kusanya mali yako katika nchi, wewe ukaaye katika mazingiwa. Maana BWANA asema hivi, Tazama, wakati huu nitawatupa wenyeji wa nchi hii kama kwa kombeo, nitawataabisha, wapate kuona taabu. Ole wangu, kwa sababu ya jeraha langu! Pigo langu laumia; lakini nilisema, Kweli, ni huzuni yangu mimi, nami sina budi kuivumilia. Hema yangu imetekwa nyara, kamba zangu zote zimekatika; watoto wangu wameniacha na kwenda zao, pia hawako. Hakuna mtu atakayenitandikia tena hema yangu, na kuyatundika mapazia yangu. Kwa sababu wachungaji wamekuwa kama wanyama, wala hawakuuliza kwa BWANA; basi hawakufanikiwa, na makundi yao yote yametawanyika. Sauti imesikiwa, Tazama, inakuja; mshindo mkuu kutoka nchi ya kaskazini, ili kuifanya miji ya Yuda kuwa ukiwa, makao ya mbweha. Ee BWANA, najua ya kuwa njia ya mwanadamu haimo katika nafsi yake; kuelekeza hatua zake si katika uwezo wa mwanadamu. Ee BWANA, unirudi kwa haki; si kwa hasira yako, usije ukaniangamiza. Hasira yako uwamwagie mataifa wasiokujua, na jamaa zao wasioliitia jina lako; kwa maana wamemla Yakobo, naam, wamemla kabisa na kumwangamiza, na kuyafanya makao yake kuwa ukiwa.
Yeremia 10:17-25 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Haya! Kusanya bidhaa yako katika nchi, wewe ukaaye katika mazingiwa. Maana BWANA asema hivi, Tazama, wakati huu nitawatupa wenyeji wa nchi hii kama kwa kombeo, nitawataabisha, wapate kuona taabu. Ole wangu, kwa sababu ya jeraha yangu! Pigo langu laumia; lakini nalisema, Kweli, ni huzuni yangu mimi, nami sina budi kuivumilia. Hema yangu umetekwa nyara, kamba zangu zote zimekatika; watoto wangu wameniacha na kwenda zao, pia hawako. Hapana mtu atakayenitandikia tena hema yangu, na kuyatundika mapazia yangu. Kwa sababu wachungaji wamekuwa kama wanyama, wala hawakuuliza kwa BWANA; basi hawakufanikiwa, na makundi yao yote yametawanyika. Sauti imesikiwa, Tazama, inakuja; mshindo mkuu kutoka nchi ya kaskazini, ili kuifanya miji ya Yuda kuwa ukiwa, makao ya mbweha. Ee BWANA, najua ya kuwa njia ya mwanadamu haimo katika nafsi yake; kuelekeza hatua zake si katika uwezo wa mwanadamu. Ee BWANA, unirudi kwa haki; si kwa hasira yako, usije ukaniangamiza. Hasira yako uwamwagie mataifa wasiokujua, na jamaa zao wasioliitia jina lako; kwa maana wamemla Yakobo, naam, wamemla kabisa na kumwangamiza, na kuyafanya makao yake kuwa ukiwa.