Waamuzi 4:1-3
Waamuzi 4:1-3 Biblia Habari Njema (BHN)
Baada ya kifo cha Ehudi, Waisraeli walitenda tena uovu mbele ya Mwenyezi-Mungu. Mwenyezi-Mungu akawatia mikononi mwa Yabini, mfalme wa Kanaani, ambaye aliishi huko Hazori. Kamanda wa jeshi lake alikuwa Sisera, mwenyeji wa Harosheth-hagoimu. Mfalme Yabini alikuwa na magari ya vita 900 ya chuma. Aliwakandamiza sana Waisraeli kwa miaka ishirini; nao wakamlilia Mwenyezi-Mungu awasaidie.
Waamuzi 4:1-3 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Hata alipokufa Ehudi, wana wa Israeli wakafanya yaliyo maovu tena mbele za macho ya BWANA. BWANA akawauza na kuwatia katika mkono wa Yabini, mfalme wa Kanaani, aliyetawala huko Hazori; na Sisera, aliyekaa katika Haroshethi wa Mataifa, alikuwa kamanda wa jeshi lake. Wana wa Israeli wakamlilia BWANA; kwa kuwa Sisera alikuwa na magari ya chuma mia tisa ya vita; naye akawakandamiza sana wana wa Israeli muda wa miaka ishirini.
Waamuzi 4:1-3 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Hata alipokufa Ehudi, wana wa Israeli wakafanya yaliyo maovu tena mbele za macho ya BWANA. BWANA akawauza na kuwatia katika mkono wa Yabini, mfalme wa Kanaani, aliyetawala huko Hazori; na Sisera, aliyekaa katika Haroshethi wa Mataifa, alikuwa amiri wa jeshi lake. Wana wa Israeli wakamlilia BWANA; kwa kuwa Sisera alikuwa na magari ya chuma mia kenda; naye akawaonea wana wa Israeli kwa nguvu muda wa miaka ishirini.
Waamuzi 4:1-3 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Baada ya Ehudi kufa, Waisraeli wakafanya tena maovu machoni pa BWANA. Hivyo BWANA akawatia mikononi mwa Yabini, mfalme wa Kanaani, aliyetawala huko Hazori. Jemadari wa jeshi lake alikuwa Sisera, aliyeishi huko Haroshethi-Hagoyimu Kwa kuwa Sisera alikuwa na magari ya chuma yapatayo 900, naye alikuwa amewatesa Waisraeli kwa ukatili kwa muda wa miaka ishirini, Waisraeli wakamlilia BWANA wakaomba msaada.