Isaya 66:12-13
Isaya 66:12-13 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Kwa kuwa hili ndilo asemalo BWANA: “Nitamwongezea amani kama mto, nao utajiri wa mataifa kama kijito kifurikacho; utanyonya na kuchukuliwa mikononi mwake na kubembelezwa magotini pake. Kama mama anavyomfariji mtoto wake, ndivyo nitakavyokufariji wewe, nawe utafarijiwa huko Yerusalemu.”
Isaya 66:12-13 Biblia Habari Njema (BHN)
Maana Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Nitakuletea fanaka nyingi kama mto, utajiri wa mataifa kama mto uliofurika. Nanyi mtanyonya na kubebwa kama mtoto mchanga, mtabembelezwa kama mtoto magotini mwa mama yake. Kama mama amtulizavyo mwanawe, kadhalika nami nitawatuliza; mtatulizwa mjini Yerusalemu.
Isaya 66:12-13 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Maana BWANA asema hivi, Tazama, nitamwelekezea amani kama mto, na utukufu wa mataifa kama kijito kifurikacho, nanyi mtapata kunyonya; mtabebwa; na juu ya magoti mtabembelezwa. Mfano wa mtu ambaye mama yake amfariji, ndivyo nitakavyowafariji ninyi; nanyi mtafarijiwa katika Yerusalemu.
Isaya 66:12-13 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)