Isaya 66:1-2
Isaya 66:1-2 Biblia Habari Njema (BHN)
Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Mbingu ni kiti changu cha enzi, dunia ni kiti cha kuwekea miguu yangu. Mtanijengea nyumba ya namna gani basi, Mahali nitakapoweza kupumzika? Mimi mwenyewe nilivifanya vitu hivi vyote, na hivi vyote ni mali yangu. Lakini ninachojali mimi ni mtu mnyenyekevu na mwenye majuto, mtu anayetetemeka asikiapo neno langu.
Isaya 66:1-2 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
BWANA asema hivi, Mbingu ni kiti changu cha enzi, na dunia ni mahali pa kuweka miguu yangu; mtanijengea nyumba ya namna gani? Na mahali pangu pa kupumzikia ni mahali gani? Maana mkono wangu ndio uliofanya hivi vyote, vitu hivi vyote vikapata kutokea, asema BWANA; lakini mtu huyu ndiye nitakayemwangalia, mtu aliye mnyonge, mwenye roho iliyopondeka, atetemekaye asikiapo neno langu.
Isaya 66:1-2 Swahili Revised Union Version (SRUV)
BWANA asema hivi, Mbingu ni kiti changu cha enzi, na dunia ni mahali pa kuweka miguu yangu; mtanijengea nyumba ya namna gani? Na mahali pangu pa kupumzikia ni mahali gani? Maana mkono wangu ndio uliofanya hivi vyote, vitu hivi vyote vikapata kutokea, asema BWANA; lakini mtu huyu ndiye nitakayemwangalia, mtu aliye mnyonge, mwenye roho iliyopondeka, atetemekaye asikiapo neno langu.
Isaya 66:1-2 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Hili ndilo asemalo BWANA, “Mbingu ni kiti changu cha enzi, nayo dunia ni mahali pa kuweka miguu yangu. Iko wapi nyumba mtakayoijenga kwa ajili yangu? Mahali pangu pa kupumzikia patakuwa wapi? Je, mkono wangu haukufanya vitu hivi vyote, hivyo vikapata kuwepo?” asema BWANA.