Isaya 60:10-14
Isaya 60:10-14 Biblia Habari Njema (BHN)
Mwenyezi-Mungu asema: “Wageni watazijenga upya kuta zako, wafalme wao watakutumikia. Maana kwa hasira yangu nilikupiga, lakini kwa fadhili yangu nimekuhurumia. Malango yako yatakuwa wazi daima; usiku na mchana hayatafungwa, ili watu wakuletee utajiri wa mataifa, pamoja na wafalme wao katika maandamano. Kila ufalme au taifa lisilokutumikia litaangamia; mataifa hayo yatatokomezwa kabisa. “Utaletewa fahari ya msitu wa Lebanoni: Mbao za miberoshi, mivinje na misonobari, zitumike kupamba mahali pa maskani yangu; nami nitaparembesha hapo ninapokaa. Wazawa wa wale waliokudhulumu, watakuja na kukuinamia kwa heshima. Wote wale waliokudharau, watasujudu mbele ya miguu yako. Watakuita: ‘Mji wa Mwenyezi-Mungu’, ‘Siyoni, Mji wa Mtakatifu wa Israeli’.
Isaya 60:10-14 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Na wageni watajenga kuta zako, Na wafalme wao watakuhudumu; Maana katika ghadhabu yangu nilikupiga, Lakini katika upendeleo wangu nimekurehemu. Malango yako nayo yatakuwa wazi daima; Hayatafungwa mchana wala usiku; Ili watu wapate kukuletea utajiri wa mataifa, Huku wakiwaongoza wafalme wao. Kwa maana kila taifa na ufalme wa watu Wasiotaka kukutumikia wataangamia; Naam, mataifa hayo wataharibiwa kabisa. Utukufu wa Lebanoni utakujia wewe, Mberoshi na mtidhari na mteashuri pamoja; Ili kupapamba mahali pangu patakatifu, Nami nitapatukuza mahali pa miguu yangu. Na wana wa watu wale waliokutesa Watakuja kwako na kukuinamia; Nao wote waliokudharau Watajiinamisha katika nyayo za miguu yako; Nao watakuita, Mji wa BWANA, Sayuni wa Mtakatifu wa Israeli.
Isaya 60:10-14 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Na wageni watajenga kuta zako, Na wafalme wao watakuhudumu; Maana katika ghadhabu yangu nalikupiga, Lakini katika upendeleo wangu nimekurehemu. Malango yako nayo yatakuwa wazi daima; Hayatafungwa mchana wala usiku; Ili watu wapate kukuletea utajiri wa mataifa, Na wafalme wao wakiongozwa pamoja nao. Kwa maana kila taifa na ufalme wa watu Wasiotaka kukutumikia wataangamia; Naam, mataifa hayo wataharibiwa kabisa. Utukufu wa Lebanoni utakujia wewe, Mberoshi na mtidhari na mteashuri pamoja; Ili kupapamba mahali pangu patakatifu, Nami nitapatukuza mahali pa miguu yangu. Na wana wa watu wale waliokutesa Watakuja kwako na kukuinamia; Nao wote waliokudharau Watajiinamisha hata nyayo za miguu yako; Nao watakuita, Mji wa BWANA, Sayuni wa Mtakatifu wa Israeli.
Isaya 60:10-14 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
“Wageni watazijenga upya kuta zako, na wafalme wao watakutumikia. Ingawa katika hasira nilikupiga, lakini katika upendeleo wangu nitakuonyesha huruma. Malango yako yatakuwa wazi siku zote, kamwe hayatafungwa, mchana wala usiku, ili watu wapate kukuletea utajiri wa mataifa: wafalme wao wakiongoza maandamano ya ushindi. Kwa maana taifa au ufalme ule ambao hautakutumikia utaangamia; utaharibiwa kabisa. “Utukufu wa Lebanoni utakujilia, msunobari, mvinje pamoja na mteashuri, ili kupapamba mahali pangu patakatifu, nami nitapatukuza mahali pa miguu yangu. Wana wa wale waliokuonea watakuja wakisujudu mbele yako, wote wanaokudharau watasujudu kwenye miguu yako, nao watakuita Mji wa BWANA, Sayuni ya Aliye Mtakatifu wa Israeli.