Isaya 59:15-16
Isaya 59:15-16 Biblia Habari Njema (BHN)
Ukweli umekosekana, naye anayeacha uovu hunyanyaswa. Mungu aliona mambo hayo, akachukizwa, alichukizwa kwamba hakuna haki. Aliona kwamba hakuna mtu aliyejali, akashangaa kwamba hakuna aliyeingilia kati. Basi akaamua kunyosha mkono wake mwenyewe, uadilifu wake ukamhimiza.
Isaya 59:15-16 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Naam, kweli imepunguka kabisa, na yeye auachaye uovu ajifanya kuwa mateka; naye BWANA akaona hayo, akachukizwa kwa kuwa hapana hukumu ya haki. Akaona ya kuwa hapana mtu, akastaajabu kwa kuwa hapana mwombezi; basi, mkono wake mwenyewe ndio uliomletea wokovu; na haki yake ndiyo iliyomsaidia.
Isaya 59:15-16 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Naam, kweli imepunguka kabisa, na yeye auachaye uovu ajifanya kuwa mateka; naye BWANA akaona hayo, akachukizwa kwa kuwa hapana hukumu ya haki. Akaona ya kuwa hapana mtu, akastaajabu kwa kuwa hapana mwombezi; basi, mkono wake mwenyewe ndio uliomletea wokovu; na haki yake ndiyo iliyomsaidia.
Isaya 59:15-16 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Kweli haipatikani popote, na yeyote aepukaye uovu huwa mawindo. BWANA alitazama naye akachukizwa kwamba hapakuwepo haki. Aliona kuwa hakuwepo hata mtu mmoja, akashangaa kwamba hakuwepo hata mmoja wa kuingilia kati; hivyo mkono wake mwenyewe ndio uliomfanyia wokovu, nayo haki yake mwenyewe ndiyo iliyomtegemeza.