Isaya 56:6-8
Isaya 56:6-8 Biblia Habari Njema (BHN)
“Watu wageni watakaonikiri mimi Mwenyezi-Mungu, watakaoniheshimu, wakapenda jina langu na kuwa watumishi wangu, wote watakaoshika Sabato bila kuikufuru, watu watakaozingatia agano langu, hao nitawaleta katika mlima wangu mtakatifu, na kuwafurahisha katika nyumba yangu ya sala; tambiko na sadaka zao zitakubaliwa madhabahuni pangu. Maana nyumba yangu itaitwa: ‘Nyumba ya sala kwa ajili ya watu wote’. “Hii ni kauli yangu mimi Bwana Mwenyezi-Mungu ninayewakusanya Waisraeli waliotawanyika. Licha ya hao niliokwisha kukusanya, nitawakusanya watu wengine wajumuike nao.”
Isaya 56:6-8 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Na wageni, walioandamana na BWANA ili wamhudumu, na kulipenda jina la BWANA, kuwa watumishi wake; kila aishikaye sabato asiivunje, na kulishika sana agano langu; Nitawaleta hao nao hadi katika mlima wangu mtakatifu, na kuwafurahisha katika nyumba yangu ya sala; makafara yao na dhabihu zao zitakubaliwa juu ya madhabahu zangu; kwa maana nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala kwa mataifa yote. Bwana MUNGU, akusanyaye waliofukuzwa katika Israeli asema, Pamoja na hayo nitamkusanyia na wengine, zaidi ya hao walio wake waliokusanywa.
Isaya 56:6-8 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Na wageni, walioandamana na BWANA ili wamhudumu, na kulipenda jina la BWANA, kuwa watumishi wake; kila aishikaye sabato asiivunje, na kulishika sana agano langu; Nitawaleta hao nao hata mlima wangu mtakatifu, na kuwafurahisha katika nyumba yangu ya sala; makafara yao na dhabihu zao zitakubaliwa juu ya madhabahu zangu; kwa maana nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala kwa mataifa yote. Bwana MUNGU, akusanyaye waliofukuzwa katika Israeli asema, Pamoja na hayo nitamkusanyia na wengine, zaidi ya hao walio wake waliokusanywa.
Isaya 56:6-8 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Wageni wanaoambatana na BWANA ili kumtumikia, kulipenda jina la BWANA, na kumwabudu yeye, wote washikao Sabato bila kuinajisi na ambao hushika sana agano langu: hawa nitawaleta kwenye mlima wangu mtakatifu na kuwapa furaha ndani ya nyumba yangu ya sala. Sadaka zao za kuteketeza na dhabihu zao zitakubalika juu ya madhabahu yangu; kwa maana nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala kwa mataifa yote.” BWANA Mwenyezi asema, yeye awakusanyaye Waisraeli waliohamishwa: “Bado nitawakusanya wengine kwao zaidi ya hao ambao wamekusanywa tayari.”