Isaya 55:11-13
Isaya 55:11-13 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
ndivyo lilivyo neno langu lile litokalo kinywani mwangu: Halitanirudia tupu, bali litatimiliza lile nililokusudia na litafanikiwa katika kusudi lile nililolituma. Mtatoka nje kwa furaha na kuongozwa kwa amani; milima na vilima vitapaza sauti kwa nyimbo mbele yenu, nayo miti yote ya shambani itapiga makofi. Badala ya kichaka cha miiba itaota miti ya misunobari, na badala ya michongoma utaota mhadasi. Hili litakuwa jambo la kumpatia BWANA jina, kwa ajili ya ishara ya milele, ambayo haitaharibiwa.”
Isaya 55:11-13 Biblia Habari Njema (BHN)
vivyo hivyo na neno langu mimi: Halitanirudia bila mafanikio, bali litatekeleza matakwa yangu, litafanikiwa lengo nililoliwekea. “Mtatoka Babuloni kwa furaha; mtaongozwa mwende kwa amani. Milima na vilima mbele yenu vitapaza sauti na kuimba, na miti yote mashambani itawapigia makofi. Badala ya michongoma kutamea misonobari, na badala ya mbigili kutamea mihadasi. Hilo litakuwa jambo litakalowakumbusha watu juu ya mambo niliyotenda mimi Mwenyezi-Mungu; ishara ya milele ambayo haitafutwa.”
Isaya 55:11-13 Swahili Revised Union Version (SRUV)
ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu; halitanirudia bure, bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma. Maana mtatoka kwa furaha, Mtaongozwa kwa amani; Mbele yenu milima na vilima vitatoa nyimbo; Na miti yote ya shambani itapiga makofi. Badala ya michongoma utamea msonobari, Na badala ya mibigili, mhadesi; Jambo hili litakuwa la kumpatia BWANA jina, Litakuwa ishara ya milele isiyokatiliwa mbali.
Isaya 55:11-13 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu; halitanirudia bure, bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma. Maana mtatoka kwa furaha, Mtaongozwa kwa amani; Mbele yenu milima na vilima vitatoa nyimbo; Na miti yote ya kondeni itapiga makofi. Badala ya michongoma utamea msunobari, Na badala ya mibigili, mhadesi; Jambo hili litakuwa la kumpatia BWANA jina, Litakuwa ishara ya milele isiyokatiliwa mbali.