Isaya 46:9-10
Isaya 46:9-10 Biblia Habari Njema (BHN)
Kumbukeni mambo niliyotenda hapo kale! Mimi ndimi Mungu na hakuna mwingine; naam, mimi ni Mungu, wala hakuna mwingine kama mimi. Nilitangaza mambo ya mwisho tangu mwanzo, tangu kale nilitangaza mambo yatakayotukia. Lengo langu litatimia; mimi nitatekeleza nia yangu yote.
Isaya 46:9-10 Swahili Revised Union Version (SRUV)
kumbukeni mambo ya zamani za kale; maana mimi ni Mungu, wala hapana mwingine; mimi ni Mungu, wala hapana aliye kama mimi; nitangazaye mwisho tangu mwanzo, na tangu zamani za kale mambo yasiyotendeka bado; nikisema, Shauri langu litasimama, nami nitatenda mapenzi yangu yote.
Isaya 46:9-10 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
kumbukeni mambo ya zamani za kale; maana mimi ni Mungu, wala hapana mwingine; mimi ni Mungu, wala hapana aliye kama mimi; nitangazaye mwisho tangu mwanzo, na tangu zamani za kale mambo yasiyotendeka bado; nikisema, Shauri langu litasimama, nami nitatenda mapenzi yangu yote.
Isaya 46:9-10 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Kumbukeni mambo yaliyopita, yale ya zamani za kale; mimi ndimi Mungu, wala hakuna mwingine; mimi ndimi Mungu, wala hakuna mwingine aliye kama mimi. Ni mimi nitangazaye mwisho tangu mwanzo, naam, tangu zamani za kale, mambo ambayo hayajatendeka. Ninasema: Kusudi langu ndilo litakalosimama, nami nitatenda mapenzi yangu yote.