Isaya 44:6-8
Isaya 44:6-8 Biblia Habari Njema (BHN)
Mwenyezi-Mungu, Mfalme na Mkombozi wa Israeli, naam, Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema hivi: “Mimi ni wa kwanza na wa mwisho; hakuna Mungu mwingine ila mimi. Ni nani Mungu aliye kama mimi? Mwache atangaze na kusema wazi mbele yangu. Nani alitangaza hapo kale mambo ambayo yatatukia? Na watuambie yale ambayo bado kutokea. Enyi watu wangu, msiogope wala msiwe na hofu, Je, sikuwaambia tangu zamani mambo yatakayotokea? Nyinyi ni mashahidi wangu. Je, yuko Mungu mwingine ila mimi? Je, kuna mwenye nguvu mwingine? Huyo simjui!”
Isaya 44:6-8 Swahili Revised Union Version (SRUV)
BWANA, Mfalme wa Israeli, Mkombozi wako, BWANA wa majeshi, asema hivi; Mimi ni wa kwanza, na mimi ni wa mwisho; zaidi yangu mimi hapana Mungu. Naye ni nani kama mimi atakayeita, na kuyahubiri haya, na kunitengenezea, tangu nilipowaweka watu wa kale? Na mambo yanayokuja na yatakayotokea, wayatangaze. Msiogope wala msifanye hofu; je! Sikukuambia haya zamani na kuyatangaza? Na ninyi ni mashahidi wangu. Je! Yuko Mungu zaidi yangu mimi? Hakika hapana Mwamba; mimi sijui mwingine.
Isaya 44:6-8 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
BWANA, Mfalme wa Israeli, Mkombozi wako, BWANA wa majeshi, asema hivi; Mimi ni wa kwanza, na mimi ni wa mwisho; zaidi yangu mimi hapana Mungu. Naye ni nani kama mimi atakayeita, na kuyahubiri haya, na kunitengenezea, tangu nilipowaweka watu wa kale? Na mambo yanayokuja na yatakayotokea, wayatangaze. Msiogope wala msifanye hofu; je! Sikukuhubiri haya zamani na kuyaonyesha? Na ninyi ni mashahidi wangu. Je! Yuko Mungu zaidi yangu mimi? Hakika hapana Mwamba; mimi sijui mwingine.
Isaya 44:6-8 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
“Hili ndilo asemalo BWANA, Mfalme wa Israeli na Mkombozi, BWANA wa majeshi: Mimi ni wa kwanza na Mimi ni wa mwisho; zaidi yangu hakuna Mungu. Ni nani basi aliye kama mimi? Yeye na atangaze. Yeye atangaze na kuweka mbele yangu ni kitu gani kilichotokea tangu nilipoumba watu wangu wa kale, tena ni nini kitakachotokea: naam, yeye na atoe unabii ni nini kitakachokuja. Msitetemeke, msiogope. Je, sikutangaza hili, na kutoa unabii tangu zamani? Ninyi ni mashahidi wangu. Je, yuko Mungu zaidi yangu mimi? Hasha, hakuna Mwamba mwingine; mimi simjui mwingine.”