Isaya 40:18-20
Isaya 40:18-20 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Basi, mtamlinganisha Mungu na nani? Au mtamfananisha na mfano wa namna gani? Sanamu fundi mmoja huiyeyusha, na mfua dhahabu huifunika dhahabu, huifulia mikufu ya fedha. Yeye aliye maskini sana hata hawezi kutoa sadaka ya namna hii, huchagua mti usiooza, hujitafutia fundi mstadi wa kusimamisha sanamu ya kuchonga isiyoweza kutikisika.
Isaya 40:18-20 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Basi, utamlinganisha Mungu na nani? Utamlinganisha na kitu gani? Kwa habari ya sanamu, fundi huisubu, naye mfua dhahabu huifunika kwa dhahabu na kuitengenezea mikufu ya fedha. Mtu aliye maskini sana asiyeweza kuleta sadaka kama hii huuchagua mti usiooza. Humtafuta fundi stadi wa kusimamisha sanamu ambayo haitatikisika.
Isaya 40:18-20 Biblia Habari Njema (BHN)
Mtamlinganisha Mungu na nini basi, au ni kitu gani cha kumfananisha naye? Je, anafanana na kinyago? Hicho, fundi hukichonga, mfua dhahabu akakipaka dhahabu, na kukitengenezea minyororo ya fedha! Au ni sanamu ya mti mgumu? Hiyo ni ukuni mtu anaochagua, akamtafuta fundi stadi, naye akamchongea sanamu imara!
Isaya 40:18-20 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Basi, mtamlinganisha Mungu na nani? Au mtamfananisha na mfano wa namna gani? Sanamu! Fundi mmoja huiyeyusha, na mfua dhahabu huifunika dhahabu, huifulia mikufu ya fedha. Yeye aliye maskini sana hata hawezi kutoa sadaka ya namna hii, huchagua mti usiooza, hujitafutia fundi stadi wa kusimamisha sanamu ya kuchonga isiyoweza kutikisika.