Isaya 40:1-5
Isaya 40:1-5 Biblia Habari Njema (BHN)
Mungu wenu asema: “Wafarijini watu wangu, nendeni mkawafariji. Semeni na wenyeji wa Yerusalemu kwa upole, waambieni kwamba utumwa wao umekwisha, wamesamehewa uovu wao. Mwenyezi-Mungu amewaadhibu maradufu kwa sababu ya dhambi zao zote.” Sauti ya mtu anaita jangwani: “Mtayarishieni Mwenyezi-Mungu njia, nyosheni barabara kuu kwa ajili ya Mungu wetu. Kila bonde litasawazishwa, kila mlima na kilima vitashushwa; ardhi isiyo sawa itafanywa sawa, mahali pa kuparuza patalainishwa. Kisha utukufu wa Mwenyezi-Mungu utafunuliwa, na watu wote pamoja watauona. Mwenyezi-Mungu mwenyewe ametamka hayo.”
Isaya 40:1-5 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Watulizeni mioyo, watulizeni mioyo, watu wangu, asema Mungu wenu. Semeni na moyo wa Yerusalemu, kauambieni kwa sauti kuu ya kwamba vita vyake vimekwisha, uovu wake umeachiliwa; kwa kuwa amepokea kwa mkono wa BWANA adhabu maradufu kwa dhambi zake zote. Sikiliza, ni sauti ya mtu aliaye, Itengenezeni nyikani njia ya BWANA; Nyosheni jangwani njia kuu kwa Mungu wetu. Kila bonde litainuliwa, Na kila mlima na kilima kitashushwa; Palipoinuka patakuwa pamenyoka, Na palipoparuza patasawazishwa; Na utukufu wa BWANA utafunuliwa, Na watu wote watauona pamoja; Kwa kuwa kinywa cha BWANA kimenena haya.
Isaya 40:1-5 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Watulizeni mioyo, watulizeni mioyo, watu wangu, asema Mungu wenu. Semeni na moyo wa Yerusalemu, kauambieni kwa sauti kuu ya kwamba vita vyake vimekwisha, uovu wake umeachiliwa; kwa kuwa amepokea kwa mkono wa BWANA adhabu maradufu kwa dhambi zake zote. Sikiliza, ni sauti ya mtu aliaye, Itengenezeni nyikani njia ya BWANA; Nyosheni jangwani njia kuu kwa Mungu wetu. Kila bonde litainuliwa, Na kila mlima na kilima kitashushwa; Palipopotoka patakuwa pamenyoka, Na palipoparuza patasawazishwa; Na utukufu wa BWANA utafunuliwa, Na wote wenye mwili watauona pamoja; Kwa kuwa kinywa cha BWANA kimenena haya.
Isaya 40:1-5 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Wafarijini, wafarijini watu wangu, asema Mungu wenu. Sema na Yerusalemu kwa upole, umtangazie kwamba kazi yake ngumu imekamilika, kwamba dhambi yake imefanyiwa fidia, kwamba amepokea kutoka mkononi mwa BWANA maradufu kwa ajili ya dhambi zake zote. Sauti ya mtu aliaye: “Itengenezeni jangwani njia ya BWANA, nyoosheni njia kuu nyikani kwa ajili ya Mungu wetu. Kila bonde litainuliwa, kila mlima na kilima kitashushwa; penye mabonde patanyooshwa, napo palipoparuza patasawazishwa. Utukufu wa BWANA utafunuliwa, nao wanadamu wote watauona pamoja. Kwa maana kinywa cha BWANA kimenena.”