Isaya 4:5-6
Isaya 4:5-6 Biblia Habari Njema (BHN)
hapo atafanya kila mahali juu ya mlima Siyoni na juu ya mikutano ya watu kuwe na wingu wakati wa mchana, na moshi na moto uwakao vizuri wakati wa usiku. Zaidi ya hayo utukufu wa Mungu utaufunika na kuulinda mji wote. Utukufu wake utakuwa kwao kivuli kuwakinga na joto la mchana; na kimbilio na kinga yao wakati wa dhoruba na mvua.
Isaya 4:5-6 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Tena juu ya makao yote ya mlima Sayuni, na juu ya makusanyiko yake, BWANA ataumba wingu na moshi wakati wa mchana, na mwangaza wa miali ya moto wakati wa usiku; kwa maana juu ya utukufu wote itatandazwa sitara. Kisha kutakuwa na hema kuwa uvuli wakati wa mchana kwa sababu ya joto, na kuwa mahali pa kukimbilia na kujificha wakati wa tufani na mvua.
Isaya 4:5-6 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Tena juu ya makao yote ya mlima Sayuni, na juu ya makusanyiko yake, BWANA ataumba wingu na moshi wakati wa mchana, na mwangaza wa miali ya moto wakati wa usiku; kwa maana juu ya utukufu wote itatandazwa sitara. Kisha kutakuwa na hema kuwa uvuli wakati wa mchana kwa sababu ya hari, na kuwa mahali pa kukimbilia na kujificha wakati wa tufani na mvua.
Isaya 4:5-6 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Kisha BWANA ataumba juu ya Mlima wote wa Sayuni, na juu ya wale wote wanaokusanyika hapo, wingu la moshi wakati wa mchana, na kungʼaa kwa miali ya moto wakati wa usiku, nako juu ya huo utukufu wote kutatanda kifuniko cha ulinzi. Utakuwa sitara na kivuli kutokana na joto la mchana, na kuwa mahali pa kujificha kutokana na dhoruba na mvua.