Isaya 35:1-2
Isaya 35:1-2 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Nyika na mahali palipo ukiwa patafurahi; jangwa litashangilia na kuchanua maua kama waridi. Litachanua maua mengi, na kufurahi, naam, kwa shangwe na kuimba; litapewa uzuri wa Lebanoni, utukufu wa Karmeli na Sharoni; watauona utukufu wa BWANA, ukuu wa Mungu wetu.
Isaya 35:1-2 Biblia Habari Njema (BHN)
Nyika na nchi kavu vitachangamka, jangwa litafurahi na kuchanua maua. Litachanua maua kwa wingi kama waridi, litashangilia na kuimba kwa furaha. Mungu atalijalia fahari ya milima ya Lebanoni, uzuri wa mlima Karmeli na wa bonde la Sharoni. Watu watauona utukufu wa Mwenyezi-Mungu, watauona ukuu wa Mungu wetu.
Isaya 35:1-2 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Nyika na mahali palipo ukiwa patafurahi; jangwa litashangilia na kuchanua maua kama waridi. Litachanua maua mengi, na kufurahi, naam, kwa shangwe na kuimba; litapewa uzuri wa Lebanoni, utukufu wa Karmeli na Sharoni; watauona utukufu wa BWANA, ukuu wa Mungu wetu.
Isaya 35:1-2 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Jangwa na nchi kame vitafurahi; nyika itashangilia na kuchanua maua. Kama waridi, litachanua maua, litashangilia sana na kupaza sauti kwa furaha. Litapewa utukufu wa Lebanoni, fahari ya Karmeli na Sharoni; wataona utukufu wa BWANA, fahari ya Mungu wetu.