Isaya 28:7-13
Isaya 28:7-13 Biblia Habari Njema (BHN)
Lakini wako wengine waliolewa divai na kuyumbayumba kwa sababu ya pombe; naam, makuhani na manabii wamelewa mvinyo, wamevurugika kwa divai. Wanayumbayumba kwa pombe kali; maono yao yamepotoka, wanapepesuka katika kutoa hukumu. Meza zote zimetapakaa matapishi, hakuna mahali popote palipo safi. Wao wananidhihaki na kuuliza: “Huyu nabii ataka kumfundisha nani? Je, anadhani atatueleza sisi ujumbe wake? Je, sisi ni watoto wachanga walioachishwa kunyonya juzijuzi? Anatufundisha kama watoto wadogo: Sheria baada ya sheria, mstari baada ya mstari; mara hiki, mara kile!” Haya basi! Mwenyezi-Mungu ataongea na watu hawa kwa njia ya watu wa lugha tofauti wanaoongea lugha ngeni. Hata hivyo yeye alikuwa amewaahidi: “Nitawaonesheni pumziko, nitawapeni pumziko enyi mliochoka. Hapa ni mahali pa pumziko.” Lakini wao hawakutaka kunisikiliza. Kwa hiyo kwao neno la Mwenyezi-Mungu litakuwa tu: Sheria sheria, mstari mstari; mara hiki, mara kile! Nao watalazimika kukimbia lakini wataanguka nyuma; watavunjika, watanaswa na kutekwa.
Isaya 28:7-13 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Lakini hawa nao wamekosa kwa divai, wamepotea kwa kileo; kuhani na nabii wamekosa kwa kileo, wamemezwa kwa divai, wamepotea kwa kileo; hukosa katika maono, hujikwaa katika hukumu. Maana meza zote zimejaa matapiko na uchafu, hapana mahali palipo safi. Atamfundisha nani maarifa? Atamfahamisha nani habari hii? Je! Ni wale walioachishwa maziwa, walioondolewa matitini? Kwa maana ni amri juu ya amri, amri juu ya amri; kanuni juu ya kanuni, kanuni juu ya kanuni; huku kidogo na huku kidogo. La, bali kwa midomo ya watu wageni, na kwa lugha nyingine atasema na watu hawa; ambao aliwaambia, Hii ndiyo raha yenu, mpeni raha yeye aliyechoka; huku ndiko kuburudika; lakini hawakutaka kusikia. Kwa sababu hiyo neno la BWANA kwao litakuwa hivi, amri juu ya amri, amri juu ya amri; kanuni juu ya kanuni, kanuni juu ya kanuni; huku kidogo na huku kidogo; ili waende na kuanguka nyuma, na kuvunjwa, na kunaswa, na kuchukuliwa.
Isaya 28:7-13 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)

Isaya 28:7-13 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Hawa pia wanapepesuka kwa sababu ya mvinyo, wanayumbayumba kwa sababu ya kileo: Makuhani na manabii wanapepesuka kwa sababu ya kileo, wanachanganyikiwa kwa sababu ya mvinyo; wanapepesuka wanapoona maono, wanajikwaa wanapotoa maamuzi. Meza zote zimejawa na matapishi wala hakuna sehemu hata ndogo isiyokuwa na uchafu. “Yeye anajaribu kumfundisha nani? Yeye anamwelezea nani ujumbe wake? Je, ni kwa watoto walioachishwa kunyonya? Je, ni wale ambao ndipo tu wametolewa matitini? Kwa maana ni: Amri juu ya amri, amri juu ya amri, kanuni juu ya kanuni, kanuni juu ya kanuni; hapa kidogo, kule kidogo.” Sawa kabisa, kwa midomo migeni na kwa lugha ngeni, Mungu atasema na watu hawa, wale ambao aliwaambia, “Hapa ni mahali pa kupumzika, waliochoka na wapumzike,” na, “Hapa ni mahali pa mapumziko,” lakini hawakutaka kusikiliza. Hivyo basi, neno la BWANA kwao litakuwa: Amri juu ya amri, amri juu ya amri, kanuni juu ya kanuni, kanuni juu ya kanuni, hapa kidogo, kule kidogo: ili waende na kuanguka chali, wakijeruhiwa, wakinaswa na kukamatwa.