Hosea 8:11-13
Hosea 8:11-13 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kwa kuwa Efraimu ameongeza madhabahu kwa dhambi, madhabahu zimekuwa dhambi kwake. Nijapomwandikia sheria yangu katika amri elfu kumi, zimehesabiwa kuwa ni kitu kigeni. Kwa habari za dhabihu za matoleo yangu, hutoa dhabihu ya nyama na kuila; lakini BWANA hawakubali; sasa ataukumbuka uovu wao, na kuwapatiliza dhambi zao; watarudi kwenda Misri.
Hosea 8:11-13 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
“Ingawa Efraimu alijenga madhabahu nyingi kwa ajili ya sadaka za dhambi, hizi zimekuwa madhabahu za kufanyia dhambi. Nimeandika kwa ajili yao mambo mengi kuhusu sheria yangu, lakini wameziangalia kama kitu cha kigeni. Wanatoa dhabihu nilizopewa mimi nao wanakula hiyo nyama, lakini BWANA hapendezwi nao. Sasa ataukumbuka uovu wao na kuadhibu dhambi zao: Watarudi Misri.
Hosea 8:11-13 Biblia Habari Njema (BHN)
“Watu wa Efraimu wamejijengea madhabahu nyingi, na madhabahu hizo zimewazidishia dhambi. Hata kama ningewaandikia sheria zangu mara nyingi, wao wangeziona kuwa kitu cha kigeni tu. Wanapenda kutoa tambiko, na kula nyama yake; lakini mimi Mwenyezi-Mungu sipendezwi hata kidogo. Mimi nayakumbuka makosa yao; nitawaadhibu kwa dhambi zao; nitawarudisha utumwani Misri.
Hosea 8:11-13 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kwa kuwa Efraimu ameongeza madhabahu kwa dhambi, madhabahu zimekuwa dhambi kwake. Nijapomwandikia sheria yangu katika amri makumi elfu, zimehesabiwa kuwa ni kitu kigeni. Kwa habari za dhabihu za matoleo yangu, hutoa dhabihu ya nyama na kuila; lakini BWANA hawakubali; sasa ataukumbuka uovu wao, na kuwapatiliza dhambi zao; watarudi kwenda Misri.