Hosea 3:1
Hosea 3:1 Biblia Habari Njema (BHN)
Mwenyezi-Mungu aliniambia, “Nenda tena ukampende mwanamke anayependwa na mwanamume mwingine na ambaye ni mzinzi. Mpende kama mimi Mwenyezi-Mungu ninavyowapenda Waisraeli, ingawa wao wanaigeukia miungu mingine na kuwa na uchu wa maandazi ya zabibu kavu.”
Hosea 3:1 Swahili Revised Union Version (SRUV)
BWANA akaniambia, Nenda tena, mpende mwanamke apendwaye na rafiki yake, naye ni mzinzi; kama vile BWANA awapendavyo wana wa Israeli, ingawa wanaigeukia miungu mingine, na kupenda mikate ya zabibu kavu.
Hosea 3:1 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
BWANA akaniambia, Enenda tena, mpende mwanamke apendwaye na rafiki yake, naye ni mzinzi; kama vile BWANA awapendavyo wana wa Israeli, ingawa wanaigeukia miungu mingine, na kupenda mikate ya zabibu kavu.
Hosea 3:1 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
BWANA akaniambia, “Nenda, ukaonyeshe upendo wako kwa mke wako tena, ingawa amependwa na mwingine naye ni mzinzi. Mpende kama BWANA apendavyo Waisraeli, ingawa wanageukia miungu mingine na kupenda mikate mitamu ya zabibu kavu iliyowekwa wakfu.”