Waebrania 1:10-12
Waebrania 1:10-12 Biblia Habari Njema (BHN)
Na tena: “Bwana, wewe uliumba dunia hapo mwanzo, mbingu ni kazi ya mikono yako. Hizo zitatoweka, lakini wewe wabaki daima, zote zitachakaa kama vazi. Utazikunjakunja kama koti, nazo zitabadilishwa kama vazi. Lakini wewe ni yuleyule daima, na maisha yako hayatakoma.”
Waebrania 1:10-12 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Na tena, Wewe, Bwana, hapo mwanzo uliitia misingi ya nchi, Na mbingu ni kazi za mikono yako; Hizo zitaharibika, bali wewe unadumu; Nazo zote zitachakaa kama nguo, Na kama mavazi utazikunjakunja, na kama mavazi zitabadilishwa; Lakini wewe u yeye yule, Na miaka yako haitakoma.
Waebrania 1:10-12 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Na tena, Wewe, Bwana, hapo mwanzo uliitia misingi ya nchi, Na mbingu ni kazi za mikono yako; Hizo zitaharibika, bali wewe unadumu; Nazo zote zitachakaa kama nguo, Na kama mavazi utazizinga, nazo zitabadilika; Lakini wewe u yeye yule, Na miaka yako haitakoma.
Waebrania 1:10-12 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Pia asema, “Hapo mwanzo, Ee Bwana, uliweka misingi ya dunia, nazo mbingu ni kazi ya mikono yako. Hizo zitatoweka, lakini wewe utadumu; zote zitachakaa kama vazi. Utazikungʼutakungʼuta kama joho, nazo zitachakaa kama vazi. Lakini wewe hubadiliki, nayo miaka yako haikomi kamwe.”