Habakuki 3:17-18
Habakuki 3:17-18 Biblia Habari Njema (BHN)
Hata kama mitini isipochanua maua, wala mizabibu kuzaa zabibu; hata kama mizeituni isipozaa zeituni, na mashamba yasipotoa chakula; hata kama kondoo wakitoweka zizini, na mifugo kukosekana mazizini, mimi nitaendelea kumfurahia Mwenyezi-Mungu nitamshangilia Mungu anayeniokoa.
Habakuki 3:17-18 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Maana mtini hautachanua maua, Wala mizabibuni hamtakuwa na matunda; Taabu ya mzeituni itakuwa bure, Na mashamba hayatatoa chakula; Zizini hamtakuwa na kundi, Wala vibandani hamtakuwa na kundi la ng'ombe; Walakini nitamfurahia BWANA Nitamshangilia Mungu wa wokovu wangu.
Habakuki 3:17-18 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Maana mtini hautachanua maua, Wala mizabibuni hamtakuwa na matunda; Taabu ya mzeituni itakuwa bure, Na mashamba hayatatoa chakula; Zizini hamtakuwa na kundi, Wala vibandani hamtakuwa na kundi la ng’ombe; Walakini nitamfurahia BWANA Nitamshangilia Mungu wa wokovu wangu.
Habakuki 3:17-18 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Ingawa mtini hauchanui maua na hakuna zabibu juu ya mizabibu, ingawaje mzeituni hauzai, na hata mashamba hayatoi chakula, iwapo hakuna kondoo katika banda, wala ngʼombe katika zizi, hata hivyo nitashangilia katika BWANA, nitamfurahia Mungu Mwokozi wangu.