Habakuki 3:1-6
Habakuki 3:1-6 Biblia Habari Njema (BHN)
Sala ya nabii Habakuki: Ee Mwenyezi-Mungu, nimesikia juu ya fahari yako, juu ya matendo yako, nami naogopa. Uyafanye tena mambo hayo wakati wetu; uyafanye yajulikane wakati huu wetu. Ukasirikapo tafadhali ukumbuke huruma yako! Mungu amekuja kutoka Temani, Mungu mtakatifu kutoka mlima Parani. Utukufu wake umetanda pote mbinguni, nayo dunia imejaa sifa zake. Mng'ao wake ni kama wa jua; miali imetoka mkononi mwake ambamo nguvu yake yadhihirishwa. Maradhi yanatangulia mbele yake, nyuma yake yanafuata maafa. Akisimama dunia hutikisika; akiyatupia jicho mataifa, hayo hutetemeka. Milima ya milele inavunjwavunjwa, vilima vya kudumu vinadidimia; humo zimo njia zake za kale na kale.
Habakuki 3:1-6 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Sala ya nabii Habakuki. Ee BWANA, nimesikia habari zako, nami naogopa; Ee BWANA, fufua kazi yako katikati ya miaka; Katikati ya miaka tangaza habari yake; Katika ghadhabu kumbuka rehema. Mungu alikuja kutoka Temani, Yeye aliye mtakatifu kutoka mlima Parani. Utukufu wake ukazifunika mbingu, Nayo dunia ikajaa sifa yake. Mwangaza wake ulikuwa kama nuru; Alikuwa na mishale ya nuru ubavuni pake; Ndipo ulipofichwa uweza wake. Mbele zake ilikwenda tauni, Na makaa ya moto yakatoka miguuni pake. Akasimama na kuitikisa dunia; Akatazama, mataifa yakatetemeka; Na milima ya zamani ikatawanyika; Vilima vya kale vikainama; Miendo yake ilikuwa kama siku za kale.
Habakuki 3:1-6 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Sala ya nabii Habakuki. Ee BWANA, nimesikia habari zako, nami naogopa; Ee BWANA, fufua kazi yako katikati ya miaka; Katikati ya miaka tangaza habari yake; Katika ghadhabu kumbuka rehema. Mungu alikuja kutoka Temani, Yeye aliye mtakatifu kutoka mlima Parani. Utukufu wake ukazifunika mbingu, Nayo dunia ikajaa sifa yake. Mwangaza wake ulikuwa kama nuru; Alikuwa na mishale ya nuru ubavuni pake; Ndipo ulipofichwa uweza wake. Mbele zake ilikwenda tauni, Na makaa ya moto yakatoka miguuni pake. Akasimama, akaitetemesha dunia; Akatazama, akawasitusha mataifa; Na milima ya zamani ikatawanyika; Vilima vya kale vikainama; Miendo yake ilikuwa kama siku za kale.
Habakuki 3:1-6 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Sala ya nabii Habakuki iliyoimbwa kwa shigionothi. BWANA, nimezisikia sifa zako; nami naogopa kwa matendo yako, Ee BWANA. Fufua kazi yako katikati ya miaka, katikati ya miaka tangaza habari yako; katika ghadhabu kumbuka rehema. Mungu alitoka Temani, yeye Aliye Mtakatifu kutoka Mlima Parani. Utukufu wake ulifunika mbingu, na sifa zake zikaifunika dunia. Mngʼao wake ulikuwa kama jua lichomozalo; mionzi ilimulika kutoka mkononi mwake, ambako nguvu zake zilifichwa. Tauni ilimtangulia; maradhi ya kuambukiza yalifuata nyayo zake. Alisimama, akaitikisa dunia; alitazama, na kuyafanya mataifa yatetemeke. Milima ya zamani iligeuka mavumbi na vilima vilivyozeeka vikaanguka. Njia zake ni za milele.