Mwanzo 38:1-11
Mwanzo 38:1-11 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ikawa wakati ule, Yuda akashuka kutoka kwa ndugu zake, akamfikia mtu Mwadulami, jina lake Hira. Yuda akaona huko binti wa mtu Mkanaani, jina lake Shua. Akamtwaa, akaingia kwake. Naye akapata mimba, akazaa mwana, akamwita jina lake Eri. Akapata mimba tena, akazaa mwana, akamwita jina lake Onani. Akaendelea, akazaa tena mwana mwingine, akamwita jina lake Shela. Naye Yuda alikuwako huko Kezibu, alipomzaa. Yuda akamwoza mke Eri, mzaliwa wake wa kwanza, na jina lake huyo mke ni Tamari. Naye Eri, mzaliwa wa kwanza wa Yuda, alikuwa mbaya machoni pa BWANA; na BWANA akamwua. Yuda akamwambia Onani, Uingie kwa mke wa nduguyo, ukamwoe, ukamwinulie nduguyo uzao. Onani alijua ya kwamba huo uzao hautakuwa wake, ikawa, alipoingia kwa mke wa nduguye, akamwagia chini asimpe nduguye uzao. Neno hili alilolifanya likawa baya machoni pa BWANA, basi akamwua yeye naye. Yuda akamwambia Tamari mkwewe, Ukae mjane nyumbani mwa baba yako hata Shela mwanangu atakapokuwa mtu mzima, maana alisema, Asipate kufa yeye kama nduguze. Basi Tamari akaenda, akakaa nyumbani mwa babaye.
Mwanzo 38:1-11 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ikawa wakati ule, Yuda akashuka kutoka kwa ndugu zake, akamfikia mtu Mwadulami, jina lake Hira. Yuda akaona huko binti wa mtu Mkanaani, jina lake Shua. Akamtwaa, akaingia kwake. Naye akapata mimba, akazaa mwana, akamwita jina lake Eri. Akapata mimba tena, akazaa mwana, akamwita jina lake Onani. Akaendelea, akazaa tena mwana mwingine, akamwita jina lake Shela. Naye Yuda alikuwa huko Kezibu, alipomzaa. Yuda akamwoza mke Eri, mzaliwa wake wa kwanza, na jina lake huyo mke ni Tamari. Naye Eri, mzaliwa wa kwanza wa Yuda, alikuwa mbaya machoni pa BWANA; na BWANA akamwua. Yuda akamwambia Onani, Uingie kwa mke wa nduguyo, ukamwoe, ukamwinulie nduguyo uzao. Onani alijua ya kwamba huo uzao hautakuwa wake, ikawa, alipoingia kwa mke wa nduguye, alimwaga mbegu chini asimpe nduguye uzao. Jambo hili alilolifanya likawa baya machoni pa BWANA, basi akamwua yeye pia. Yuda akamwambia Tamari mkwewe, Ukae mjane nyumbani mwa baba yako hata Shela mwanangu atakapokuwa mtu mzima, maana alisema, Asipate kufa yeye kama nduguze. Basi Tamari akaenda, akakaa nyumbani mwa babaye.
Mwanzo 38:1-11 Biblia Habari Njema (BHN)
Wakati huo, Yuda alitengana na ndugu zake, akaenda kukaa na mtu mmoja Mwadulami, jina lake Hira. Akiwa huko, Yuda akamwona binti Shua, Mkanaani, akamwoa. Binti Shua akapata mimba akazaa mtoto wa kiume, Yuda akamwita Eri. Akapata mimba nyingine, akajifungua mtoto wa kiume, akamwita Onani. Kisha akapata mtoto mwingine wa kiume, akamwita Shela. Wakati Shela alipozaliwa, Yuda alikuwa Kezibu. Baadaye Yuda alimwoza mtoto wake wa kwanza Eri, kwa mwanamke aitwaye Tamari. Lakini Eri, mzaliwa wa kwanza wa Yuda, alikuwa mwovu mbele ya Mwenyezi-Mungu; hivyo Mwenyezi-Mungu akamuua. Basi, Yuda akamwambia Onani, “Mchukue mke wa ndugu yako marehemu, kwani ndivyo inavyokupasa kufanya, upate kumzalia nduguyo watoto.” Lakini Onani alijua kwamba hao watoto wasingekuwa wake. Kwa hiyo, alipolala na mke wa nduguye, alimwaga chini mbegu ya uzazi, asije akampatia nduguye watoto. Tendo hilo likamwudhi Mwenyezi-Mungu, akamuua Onani pia. Ndipo Yuda akamwambia Tamari, mke wa mwanawe, “Rudi nyumbani kwa baba yako, ubaki mjane hadi mwanangu Shela atakapokua.” Yuda alihofu Shela naye asije akafa kama ndugu zake. Basi, Tamari akarudi nyumbani kwa baba yake.
Mwanzo 38:1-11 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)
Wakati ule, Yuda akawaacha ndugu zake, akaenda kuishi na Hira Mwadulami. Huko Yuda akakutana na binti ya Mkanaani aitwaye Shua. Akamwoa na akakutana naye kimwili, naye akapata mimba, na akamzaa mwana, aliyeitwa jina Eri. Akapata mimba tena, akamzaa mwana na kumwita jina Onani. Akamzaa mwana mwingine tena, akamwita jina Shela. Huyu alimzalia huko Kezibu. Yuda akamtwalia Eri, mzaliwa wake wa kwanza, mke aliyeitwa Tamari. Lakini Eri, mzaliwa wa kwanza wa Yuda, alikuwa mwovu machoni pa Mwenyezi Mungu, kwa hiyo Mwenyezi Mungu akamuua. Kisha Yuda akamwambia Onani, “Kutana kimwili na mke wa ndugu yako, na utimize wajibu wako kwake kama mke wa ndugu yako, ili umpatie ndugu yako uzao.” Lakini Onani alijua kwamba uzao haungekuwa wake, kwa hiyo kila alipokutana kimwili na mke wa ndugu yake, alimwaga mbegu chini ili asimpatie ndugu yake uzao. Alichofanya kilikuwa kiovu machoni pa Mwenyezi Mungu, hivyo Mwenyezi Mungu akamuua Onani pia. Kisha Yuda akamwambia Tamari mkwewe, “Ishi kama mjane nyumbani mwa baba yako hadi mwanangu Shela atakapokua.” Kwa maana alifikiri, “Anaweza kufa pia kama ndugu zake.” Kwa hiyo Tamari akaenda kuishi nyumbani mwa baba yake.