Mwanzo 18:18-19
Mwanzo 18:18-19 Biblia Habari Njema (BHN)
Yeye atakuwa baba wa taifa kubwa na kwake mataifa yote ya ulimwengu yatabarikiwa! Nimemchagua yeye na wazawa wake. Yeye atawafunza wazawa wake kushika njia yangu: Wawe waadilifu na wenye kutenda mambo ya haki, nami nipate kuwatimizia ahadi zangu.
Mwanzo 18:18-19 Swahili Revised Union Version (SRUV)
ikiwa Abrahamu atakuwa taifa kuu, hodari, na katika yeye mataifa yote ya dunia watabarikiwa? Kwa maana nimemchagua ili awaamuru wanawe na vizazi vyake baada yake wadumishe njia ya BWANA, kwa kuwa wenye haki na kweli, ili BWANA naye akamtimizie Abrahamu ahadi zake.
Mwanzo 18:18-19 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
akiwa Ibrahimu atakuwa taifa kuu, hodari, na katika yeye mataifa yote ya dunia watabarikiwa? Kwa maana nimemjua ya kwamba atawaamuru wanawe, na nyumba yake baada yake waishike njia ya BWANA, wafanye haki na hukumu, ili kwamba BWANA naye akamtimizie Ibrahimu ahadi zake.
Mwanzo 18:18-19 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Hakika Abrahamu atakuwa taifa kubwa na lenye nguvu, kupitia kwake mataifa yote ya dunia yatabarikiwa. Kwa maana nimemchagua yeye, ili awaongoze watoto wake na jamaa yake kufuata njia ya BWANA, kwa kuwa waadilifu na kutenda haki, ili BWANA atimize ahadi yake kwa Abrahamu.”