Ezra 3:1-3
Ezra 3:1-3 Biblia Habari Njema (BHN)
Baadaye mwezi wa saba ulipofika, na watu wa Israeli wakiwa wamekwisha kaa katika miji yao, wote walikusanyika pamoja mjini Yerusalemu. Yeshua, mwana wa Yosadaki, pamoja na makuhani wenzake, na Zerubabeli, mwana wa Shealtieli, pamoja na jamaa zake, waliijenga upya madhabahu ya Mungu wa Israeli, ili waweze kumtolea sadaka za kuteketezwa kama ilivyoandikwa katika sheria ya Mose, mtu wa Mungu. Waliijenga madhabahu hiyo mahali palepale ilipokuwa hapo zamani, kwa kuwa waliwaogopa watu waliokuwa wanaishi katika nchi hiyo. Kisha wakawa wanamtolea Mwenyezi-Mungu sadaka za kuteketezwa juu yake kila siku asubuhi na jioni.
Ezra 3:1-3 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Hata ulipowadia mwezi wa saba, na wana wa Israeli walipokuwa katika miji yao, watu wakakusanyika pamoja huko Yerusalemu. Ndipo akasimama Yoshua, mwana wa Yosadaki, na ndugu zake makuhani, na Zerubabeli, mwana wa Shealtieli, na ndugu zake, nao wakaijenga madhabahu ya Mungu wa Israeli, ili kutoa sadaka za kuteketezwa juu yake, kama ilivyoandikwa katika Torati ya Musa, mtu wa Mungu. Wakaiweka madhabahu juu ya msingi wake; maana hofu imewashika kwa sababu ya watu wa nchi; wakamtolea BWANA sadaka za kuteketezwa juu yake, sadaka za kuteketezwa za asubuhi na jioni.
Ezra 3:1-3 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Hata ulipowadia mwezi wa saba, na wana wa Israeli walipokuwa katika miji yao, watu wakakusanyika pamoja huko Yerusalemu kama mtu mmoja. Ndipo akasimama Yoshua, mwana wa Yosadaki, na ndugu zake makuhani, na Zerubabeli, mwana wa Shealtieli, na ndugu zake, nao wakaijenga madhabahu ya Mungu wa Israeli, ili kutoa sadaka za kuteketezwa juu yake, kama ilivyoandikwa katika torati ya Musa, mtu wa Mungu. Wakaiweka madhabahu juu ya msingi wake; maana hofu imewashika kwa sababu ya watu wa nchi; wakamtolea BWANA sadaka za kuteketezwa juu yake, sadaka za kuteketezwa za asubuhi na jioni.
Ezra 3:1-3 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Mwezi wa saba ulipowadia baada ya Waisraeli kukaa katika miji yao, watu wote walikusanyika huko Yerusalemu kama mtu mmoja. Yeshua mwana wa Yosadaki na makuhani wenzake, Zerubabeli mwana wa Shealtieli pamoja na wenzake walianza kujenga madhabahu ya Mungu wa Israeli ili kumtolea dhabihu za sadaka za kuteketezwa kwa moto juu yake, kulingana na ilivyoandikwa katika Sheria ya Mose mtu wa Mungu. Ingawa waliwaogopa watu waliowazunguka, walijenga madhabahu juu ya ule msingi wake, wakamtolea BWANA dhabihu za sadaka za kuteketezwa kwa moto juu yake za asubuhi na za jioni.