Ezekieli 3:1-3
Ezekieli 3:1-3 Biblia Habari Njema (BHN)
Akaniambia, “Wewe mtu, kula unachopewa; kula kitabu hiki kisha uende ukawaeleze Waisraeli.” Kwa hiyo nilifumbua kinywa changu, naye akanilisha hicho kitabu. Halafu akaniambia, “Wewe mtu, kula kitabu hiki ninachokupa, ujaze tumbo lako.” Basi, nilikula kitabu hicho, nacho kikawa kitamu mdomoni kama asali.
Ezekieli 3:1-3 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Akaniambia, Mwanadamu, kula uonacho; kula gombo hili, kisha nenda ukaseme na wana wa Israeli. Basi nikafunua kinywa changu, naye akanilisha lile gombo. Akaniambia, Mwanadamu, lisha tumbo lako, ulijaze tumbo lako kwa hili gombo nikupalo. Ndipo nikalila, nalo kinywani mwangu lilikuwa tamu, kama utamu wa asali.
Ezekieli 3:1-3 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Akaniambia, Mwanadamu, kula uonacho; kula gombo hili, kisha enenda ukaseme na wana wa Israeli. Basi nikafunua kinywa changu, naye akanilisha lile gombo. Akaniambia, Mwanadamu, lisha tumbo lako, ulijaze tumbo lako kwa hili gombo nikupalo. Ndipo nikalila, nalo kinywani mwangu lilikuwa tamu, kama utamu wa asali.
Ezekieli 3:1-3 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Naye akaniambia, “Mwanadamu, kula kile kilichoko mbele yako, kula huu ukurasa wa kitabu, kisha uende ukaseme na nyumba ya Israeli.” Ndipo nikafungua kinywa changu, naye akanilisha ule ukurasa wa kitabu. Ndipo akaniambia, “Mwanadamu, kula ukurasa huu wa kitabu ninaokupa ujaze tumbo lako.” Kwa hiyo nikaula, ulikuwa mtamu kama asali kinywani mwangu.