Ezekieli 15:1-8
Ezekieli 15:1-8 Biblia Habari Njema (BHN)
Neno la Mwenyezi-Mungu lilinijia: “Wewe mtu! Je, mti wa mzabibu ni bora kuliko miti mingine msituni? Je, mti wake wafaa kutengenezea kitu chochote? Je, watu huweza kutengeneza kigingi kutoka mti huo ili waweze kutundikia vitu? Huo wafaa tu kuwashia moto. Tena moto unapoteketeza sehemu yake ya mwanzo na ya mwisho na kuikausha sehemu ya katikati, je, hiyo yafaa kwa kitu chochote? Ulipokuwa haujachomwa ulikuwa haufai kitu, sembuse sasa baada ya kuteketezwa kwa moto na kuwa makaa! Haufai kitu kabisa. Basi, mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Kama vile nilivyoutoa mti wa mzabibu kati ya miti ya msituni, ukateketezwa motoni, ndivyo nilivyotoa wakazi wa Yerusalemu. Nitawakabili vikali. Hata kama wataukimbia moto, huo moto utawateketeza. Hapo nitakapowakabili vikali, ndipo mtakapotambua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu. Kwa kuwa wamekosa uaminifu kwangu, nitaifanya nchi yao kuwa ukiwa. Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nimesema.”
Ezekieli 15:1-8 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Neno la BWANA likanijia, kusema, Mwanadamu, mzabibu una sifa gani kuliko mti mwingine, au tawi la mzabibu lililokuwa kati ya miti ya msituni? Je! Mti wake waweza kutwaliwa, ili kufanya kazi yoyote? Watu waweza kufanya chango kwa huo, ili kutundika chombo chochote? Tazama, watupwa motoni kuwa kuni moto unapoziteketeza ncha zake zote mbili, nao umeteketea katikati, je! Wafaa kwa kazi yoyote? Tazama, ulipokuwa mzima, haukufaa kwa kazi yoyote; sembuse ukiisha kuliwa na moto, na kuteketea; je! Waweza kufaa kwa kazi yoyote? Basi Bwana MUNGU asema hivi; Kama mzabibu kati ya miti ya msituni, niliyoupa moto uwe kuni, ndivyo nitakavyowatoa wakaao Yerusalemu. Nami nitaukaza uso wangu juu yao; nao watatoka motoni, lakini moto utawateketeza; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi BWANA, nitakapoukaza uso wangu juu yao. Nami nitaifanya nchi kuwa ukiwa, kwa sababu wamekosa, asema Bwana MUNGU.
Ezekieli 15:1-8 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Neno la BWANA likanijia, kusema, Mwanadamu, mzabibu una sifa gani kuliko mti mwingine, au tawi la mzabibu lililokuwa kati ya miti ya msituni? Je! Mti wake waweza kutwaliwa, ili kufanya kazi yo yote? Watu waweza kufanya chango kwa huo, ili kutundika chombo cho chote? Tazama, watupwa motoni kwa kuni moto umeziteketeza ncha zake zote mbili, nao umeteketea katikati, je! Wafaa kwa kazi yo yote? Tazama, ulipokuwa mzima, haukufaa kwa kazi yo yote; sembuse ukiisha kuliwa na moto, na kuteketea; je! Waweza kufaa kwa kazi yo yote? Basi Bwana MUNGU asema hivi; Kama mzabibu kati ya miti ya msituni, niliyoupa moto uwe kuni, ndivyo nitakavyowatoa wakaao Yerusalemu. Nami nitaukaza uso wangu juu yao; nao watatoka motoni, lakini moto utawateketeza; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi BWANA, nitakapoukaza uso wangu juu yao. Nami nitaifanya nchi kuwa ukiwa, kwa sababu wamekosa, asema Bwana MUNGU.
Ezekieli 15:1-8 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)
Neno la Mwenyezi Mungu likanijia kusema: “Mwanadamu, je, ni vipi mti wa mzabibu unaweza kuwa bora kuliko tawi la mti mwingine wowote ndani ya msitu? Je, mti wake kamwe huchukuliwa na kutengeneza chochote cha manufaa? Je, watu hutengeneza vigingi vya kuning’inizia vitu kutokana na huo mti wake? Nao baada ya kutiwa motoni kama nishati na moto ukateketeza ncha zote mbili na kuunguza sehemu ya kati, je, unafaa kwa lolote? Kama haukufaa kitu chochote ulipokuwa mzima, je, si zaidi sana sasa ambapo hauwezekani kufanyishwa chochote cha kufaa baada ya moto kuuchoma na kuuacha majivu? “Kwa hiyo hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Kama nilivyoutoa mti wa mzabibu miongoni mwa miti ya msituni kuwa nishati ya moto, hivyo ndivyo nitakavyowatendea watu wanaoishi Yerusalemu. Nitaukaza uso wangu dhidi yao. Ingawa watakuwa wameokoka kwenye moto, bado moto utawateketeza. Nitakapoukaza uso wangu dhidi yao, ninyi mtajua kuwa Mimi ndimi Mwenyezi Mungu. Nitaifanya nchi kuwa ukiwa kwa sababu wamekuwa si waaminifu, asema Bwana Mungu Mwenyezi.”