Kutoka 6:26-30
Kutoka 6:26-30 Biblia Habari Njema (BHN)
Aroni na Mose ndio walioambiwa na Mwenyezi-Mungu, “Watoeni watu wa Israeli kutoka nchi ya Misri, vikundi kwa vikundi.” Ndio haohao Mose na Aroni walioongea na Farao, mfalme wa Misri, juu ya kuwatoa Waisraeli nchini Misri. Siku ile Mwenyezi-Mungu alipoongea na Mose nchini Misri, alimwambia, “Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu. Mwambie Farao, mfalme wa Misri, maneno yote ninayokuambia.” Lakini Mose akamwambia Mwenyezi-Mungu, “Mimi sina ufasaha wa kuongea; Farao atanisikilizaje?”
Kutoka 6:26-30 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Hawa ni Haruni yeye yule, na Musa yeye yule, BWANA aliowaambia, akisema, Watoeni wana wa Israeli watoke nchi ya Misri sawasawa na majeshi yao. Ni hao walionena na Farao mfalme wa Misri ili wawatoe wana wa Israeli watoke Misri; hao ni Musa yeye yule, na Haruni yeye yule. Ilikuwa siku hiyo BWANA aliponena na Musa katika nchi ya Misri, BWANA akamwambia Musa, akasema, Mimi ni BWANA; mwambie Farao mfalme wa Misri maneno yote nikuambiayo. Musa akanena mbele ya BWANA, Mimi ni mtu mwenye midomo isiyo tohara, Farao atanisikizaje?
Kutoka 6:26-30 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Hawa ni Haruni ye yule, na Musa ye yule, BWANA aliowaambia, akisema, Watoeni wana wa Israeli watoke nchi ya Misri sawasawa na majeshi yao. Ni hao walionena na Farao mfalme wa Misri ili wawatoe wana wa Israeli watoke Misri; hao ni Musa ye yule, na Haruni ye yule. Ilikuwa siku hiyo BWANA aliponena na Musa katika nchi ya Misri, BWANA akamwambia Musa, akasema, Mimi ni BWANA; mwambie Farao mfalme wa Misri maneno yote nikuambiayo. Musa akanena mbele ya BWANA, Mimi ni mtu mwenye midomo isiyo tohara, Farao atanisikizaje?
Kutoka 6:26-30 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Hawa walikuwa Aroni na Mose wale wale ambao BWANA aliwaambia, “Watoeni Waisraeli katika nchi ya Misri kwa vikosi vyao.” Ndio hao hao waliozungumza na Farao mfalme wa Misri kuhusu kuwatoa Waisraeli Misri. Ilikuwa ni huyo Mose na huyo Aroni. BWANA aliponena na Mose huko Misri, akamwambia, “Mimi ndimi BWANA. Mwambie Farao mfalme wa Misri kila kitu nikuambiacho.” Lakini Mose akamwambia BWANA, “Kwa kuwa mimi huzungumza kwa kigugumizi, Farao atanisikiliza mimi?”