Kutoka 1:20-21
Kutoka 1:20-21 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Basi Mungu akawatendea mema wale wazalisha; na hao watu wakaongezeka sana, wakaendelea na kuzidi kuwa na nguvu nyingi. Ilikuwa kwa sababu wale wazalisha walikuwa wakimcha Mungu, akawasimamishia nyumba.
Shirikisha
Soma Kutoka 1Kutoka 1:20-21 Biblia Habari Njema (BHN)
Basi, Mungu akawajalia mema wakunga hao, nao Waisraeli wakazidi kuongezeka na kuwa na nguvu sana. Na kwa vile wakunga hao walimcha Mungu, Mungu akawajalia kupata jamaa zao wenyewe.
Shirikisha
Soma Kutoka 1