Kutoka 1:15-16
Kutoka 1:15-16 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kisha mfalme wa Misri akawaambia wakunga wa Waebrania, mmoja jina lake aliitwa Shifra, na wa pili jina lake aliitwa Pua; akasema, Wakati mnapowazalisha wanawake wa Kiebrania na kuona kuwa ni mtoto wa kiume basi mwueni, bali ikiwa ni mtoto wa kike, na aishi.
Kutoka 1:15-16 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kisha mfalme wa Misri akasema na wazalisha wa Waebrania, mmoja jina lake aliitwa Shifra, na wa pili jina lake aliitwa Pua; akasema, Wakati mwazalishapo wanawake wa Kiebrania na kuwaona wa katika kuzaa, ikiwa ni mtoto mwanamume, basi mwueni, bali ikiwa ni mtoto mwanamke, na aishi.
Kutoka 1:15-16 Biblia Habari Njema (BHN)
Kisha, mfalme wa Misri akawaambia wakunga wa Misri, Shifra na Pua, ambao waliwahudumia wanawake wa Kiebrania, “Mnapowahudumia wanawake wa Kiebrania wanapojifungua, ikiwa mtoto anayezaliwa ni wa kiume, muueni. Lakini ikiwa ni wa kike, mwacheni aishi.”
Kutoka 1:15-16 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Mfalme wa Misri akawaambia wakunga wa Kimisri waliowazalisha wanawake wa Kiebrania, ambao majina yao ni Shifra na Pua, “Mtakapowazalisha wanawake wa Kiebrania, chunguzeni wanapojifungua. Ikiwa ni mtoto wa kiume, muueni, lakini ikiwa ni msichana, mwacheni aishi.”