Esta 10:1-2
Esta 10:1-2 Biblia Habari Njema (BHN)
Mfalme Ahasuero alitoza kodi watu wa bara na pwani. Matendo yake yote makuu na ya ajabu, pamoja na simulizi kamili kuhusu jinsi alivyompandisha cheo Mordekai na kumtunukia heshima kuu, yote yameandikwa katika Kitabu cha Kumbukumbu za wafalme wa Media na Persia.
Esta 10:1-2 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Basi mfalme Ahasuero alitoza kodi katika nchi na katika visiwa vya bahari. Na matendo yake yote yenye nguvu na ya ushujaa, na habari zote za ukuu wake Mordekai ambao alipewa na mfalme, hazikuandikwa katika Kitabu cha Kumbukumbu za Wafalme wa Umedi na Uajemi?
Esta 10:1-2 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Basi mfalme Ahasuero alitoza kodi katika nchi na katika visiwa vya bahari. Na matendo yake yote yenye nguvu na ya ushujaa, na habari zote za ukuu wake Mordekai ambao alipewa na mfalme, hazikuandikwa katika kitabu-cha-taarifa cha wafalme wa Umedi na Uajemi?
Esta 10:1-2 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Mfalme Ahasuero alitoza ushuru katika ufalme wake wote hadi kwenye miambao yake ya mbali. Matendo yake yote ya nguvu na uwezo, pamoja na habari zote za ukuu wa Mordekai ambao mfalme alikuwa amemkuza, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Umedi na Uajemi?