Waefeso 2:4-6
Waefeso 2:4-6 Biblia Habari Njema (BHN)
Lakini Mungu ni mwenye huruma nyingi. Alitupenda kwa mapendo yasiyopimika, hata, ingawa tulikuwa tumekufa kwa sababu ya dhambi, alitufanya hai pamoja na Kristo. Kwa neema ya Mungu nyinyi mmeokolewa. Kwa kuungana na Kristo Yesu, Mungu alitufufua pamoja naye, tukatawale pamoja naye mbinguni.
Waefeso 2:4-6 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Lakini Mungu, kwa kuwa ni mwingi wa rehema, kwa mapenzi yake makuu aliyotupenda; hata wakati ule tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu; alitufanya kuwa hai pamoja na Kristo; yaani, tumeokolewa kwa neema. Akatufufua pamoja naye, akatuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa roho, katika Kristo Yesu
Waefeso 2:4-6 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Lakini Mungu, kwa kuwa ni mwingi wa rehema, kwa mapenzi yake makuu aliyotupenda; hata wakati ule tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu; alituhuisha pamoja na Kristo; yaani, tumeokolewa kwa neema. Akatufufua pamoja naye, akatuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa roho, katika Kristo Yesu
Waefeso 2:4-6 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Lakini Mungu kwa upendo wake mwingi kwetu sisi, ambaye ni mwingi wa rehema, hata tulipokuwa wafu kwa ajili ya makosa yetu, alitufanya tuwe hai pamoja na Kristo Yesu, yaani, mmeokolewa kwa neema. Mungu alitufufua pamoja na Kristo na kutuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa roho katika Kristo Yesu