Kumbukumbu la Sheria 8:10-11
Kumbukumbu la Sheria 8:10-11 Biblia Habari Njema (BHN)
Mtakula na kushiba, mtamshukuru Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, kwa nchi nzuri aliyowapa. “Hakikisheni kwamba hamtamsahau Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, kwa kutoshika amri zake, maagizo yake na masharti yake ninayowaamuru leo.
Kumbukumbu la Sheria 8:10-11 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Nawe utakula ushibe, utamshukuru BWANA, Mungu wako, kwa nchi nzuri aliyokupa. Jihadhari, usije ukamsahau BWANA, Mungu wako, kwa kutozishika amri zake, na hukumu zake, na sheria zake, ninazokuamuru leo.
Kumbukumbu la Sheria 8:10-11 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Nawe utakula ushibe, utamshukuru BWANA, Mungu wako, kwa nchi nzuri aliyokupa. Jihadhari, usije ukamsahau BWANA, Mungu wako, kwa kutozishika amri zake, na hukumu zake, na sheria zake, ninazokuamuru leo.
Kumbukumbu la Sheria 8:10-11 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Wakati mtakapokwisha kula na kushiba, msifuni BWANA Mungu wenu kwa ajili ya nchi nzuri aliyowapa. Jihadharini msimsahau BWANA Mungu wenu, mkashindwa kushika maagizo yake, sheria na amri zake ambazo ninawapa leo.