Kumbukumbu la Sheria 5:1-5
Kumbukumbu la Sheria 5:1-5 Biblia Habari Njema (BHN)
Mose aliwaita pamoja Waisraeli, akawaambia: “Enyi Waisraeli, sikilizeni masharti na maagizo ambayo ninayatamka mbele yenu leo. Jifunzeni hayo na kuyatekeleza kwa uangalifu. Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, alifanya agano nasi mlimani Horebu. Hakufanya agano hilo na wazee wetu tu, bali alifanya na sisi sote ambao tuko hai hivi leo. Mwenyezi-Mungu aliongea nanyi ana kwa ana huko mlimani katikati ya moto. Wakati huo mimi nilisimama kati yenu na Mwenyezi-Mungu, nikawatangazieni yale aliyoyasema, kwa kuwa nyinyi mliogopa ule moto na hamkupanda mlimani. Mwenyezi-Mungu alisema hivi
Kumbukumbu la Sheria 5:1-5 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Musa akawaita Israeli wote, akawaambia, Enyi Israeli, zisikieni amri na hukumu nisemazo masikioni mwenu leo, mpate kujifunza na kuzizingatia. BWANA, Mungu wetu, alifanya agano nasi katika Horebu. BWANA hakufanya agano hili na baba zetu, bali na sisi, yaani, sisi sote tuliopo hapa, tu hai. BWANA alisema nanyi uso kwa uso mlimani, kutoka kati ya moto; (nami wakati ule nikiwa nimesimama kati ya BWANA na ninyi, ili kuwaonesha neno la BWANA; maana, mliogopa kwa sababu ya ule moto, wala hamkupanda mlimani); naye akasema
Kumbukumbu la Sheria 5:1-5 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Musa akawaita Israeli wote, akawaambia, Enyi Israeli, zisikieni amri na hukumu ninenazo masikioni mwenu leo, mpate kujifunza na kuangalia kuzitenda. BWANA, Mungu wetu, alifanya agano nasi katika Horebu. BWANA hakufanya agano hili na baba zetu, bali na sisi, yaani, sisi sote tuliopo hapa, tu hai. BWANA alisema nanyi uso kwa uso mlimani, toka kati ya moto; (nami wakati ule nalisimama kati ya BWANA na ninyi, ili kuwaonyesha neno la BWANA; maana, mliogopa kwa sababu ya ule moto, wala hamkupanda mlimani); naye akasema
Kumbukumbu la Sheria 5:1-5 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Mose akawaita Israeli wote, akawaambia: Ee Israeli, sikilizeni amri na sheria ninazowatangazia leo. Jifunzeni, na mwe na hakika kuzifuata. BWANA Mungu wetu alifanya Agano nasi katika mlima wa Horebu. Si kwamba BWANA alifanya Agano na baba zetu, bali alifanya nasi, nasi sote ambao tuko hai hapa leo. BWANA alisema nanyi uso kwa uso kutoka moto juu ya mlima. (Wakati huo nilisimama kati ya BWANA na ninyi kuwatangazia neno la BWANA, kwa sababu mliogopa ule moto, nanyi hamkupanda mlimani.) Naye Mungu alisema