Kumbukumbu la Sheria 33:29
Kumbukumbu la Sheria 33:29 Biblia Habari Njema (BHN)
Heri yenu nyinyi Waisraeli. Nani aliye kama nyinyi, watu mliookolewa na Mwenyezi-Mungu, ambaye ndiye ngao ya msaada wenu, na upanga unaowaletea ushindi! Adui zenu watakuja wananyenyekea mbele yenu, nanyi mtawakanyaga chini.”
Kumbukumbu la Sheria 33:29 Swahili Revised Union Version (SRUV)
U heri, Israeli. Ni nani aliye kama wewe, taifa lililookolewa na BWANA! Ndiye ngao ya msaada wako, Na upanga wa utukufu wako; Na adui zako watajitiisha chini yako, Nawe utapakanyaga mahali pao pa juu.
Kumbukumbu la Sheria 33:29 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
U heri, Israeli. Ni nani aliye kama wewe, taifa lililookolewa na BWANA! Ndiye ngao ya msaada wako, Na upanga wa utukufu wako; Na adui zako watajitiisha chini yako, Nawe utapakanyaga mahali pao pa juu.
Kumbukumbu la Sheria 33:29 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Ee Israeli, wewe umebarikiwa! Ni nani kama wewe, taifa lililookolewa na BWANA? Yeye ni ngao yako na msaada wako, na upanga wako uliotukuka. Adui zako watatetemeka mbele yako, nawe utapakanyaga mahali pao pa juu.”